sasa hivi kuna Team ZariMondi na Team Wema Sepetu kuna mengi yametokea hapo kati na bado yanaendelea,
Inasemekana Diamond na Zari walikutana ndani ya ndege kati ya mwezi October na November 2014 wakati Diamond akirudi kutoka kwa mzee madiba Afrika kusini na mwanadada Zari naye alikua anakuja Tzee kuonana na Pedeshee flani aliyekua tayari kishamlipia gharama za ndege na hoteli,
Zari akiwa amezishika Tuzo Za Diamond alizoshinda kwenye Channel O |
si anamwonaga kwenye ma Tv, mchizi akaenda kukaa kwenye siti yake ambayo pembeni ilikua haina mtu na nyuma yake alikua ametulia mtoto mzuri Zari nae pembeni yake kulikua kutupu, Mondi akakaa na kuvaa headphone zake, mwanadada uzalendo ukamshinda akamgusa D begani na kumsemesha kiganda kumsalimia kisha akamkaribisha jamaa akaribie siti ya nyuma D (Zaaaali la mentaaaali) hakusita akaja siti ya nyuma, kilichoendelea baada ya hapo...... kufikia Jk Nyerere Airport Zari akatemana na ahadi yake ya kukutana na Pedeshee wa Dsm na kuungana na Diamond ambaye alimsindikiza Zari kwenye Hoteli nyingine wakaanza kula zao rahaaaaaa, kilichoendelea baada ya hapo ..... Ungana na Soudy Brown anaelezea mahusiana haya tangu yanaanza mpaka yalipo kwa wakati huu na Gossip Cop Tz ameenda mbali zaidi kwa kupiga story na mashabiki wa pande hizo mbili ndani ya Power Break Fast ya Clouds fm...