Thursday, January 15, 2015
FLAVIANA MATATA "NDOA HAITAATHIRI KAZI YANGU"
Mwanamitindo Flaviana Matata ambaye alichumbiwa Novemba 2014 amesema kuwa ndoa haitaathiri kazi zake...
Akiongea na XXL Clouds Fm Radio, Flavi amesema
"Kila kitu kitaendelea kama kilivyo hadi hapo ntakapoona sasa imetosha nifanye mambo mengine, lakini haitabadilisha chochote , itabadilisha status tu ndo inakuwa Mrs flani basi"
Flaviana hufanya shughuli zake Marekani na amesema kuwa anaolewa na mtanzania anaeishi marekani lakini hajamtaja jina...
Maelezo yake ya kwanini ameamua kuolewa na mtanzania ni kuwa...
"Utamaduni ni muhimu sana, kwakweli simzuii mtu kuolewa na utamaduni wowote lakini mimi ninajua ninachiokihitaji katika maisha yangu, najua hatufanani mwingine anataka mzungu, mwengine muhindi lakini mimi cha kwanza kabisa, utamaduni ni muhimu"
Comments System
facebook