Wednesday, April 15, 2015

SIMANZI: WARAKA WA MABESTE KWA WATANZANIA


Usiku wa manane kuamkia siku ya leo Rapper Mabeste kupitia kwenye account yake ya instagram ameandika waraka mzito kutoka moyoni mwake akielezea magumu anayopitia wakati huu baada ya kuwa anamuuguza mke wake mtarajiwa aliyemzalia mtoto mmoja, waraka huo unasomeka kama ifuatavyo:-


PART 1.

Hii ni kwa waTanzania wenzangu, ndugu zangu na fans wote wa Mabeste!! Watu husema mficha maradhi kifo humuumbua!! Mke wangu anaumwa mda mref tangia ana ujauzito wa mtoto wetu (kendrick) alikua akisumbuliwa na moyo unakua unamuuma, pumzi zinabana! Na alikua anazimia zimia mara kwa mara! Hospital wakasema itakua ni ujauzito unamsumbua!! Na alikua akipimwa pressure inakua low! Mungu alimlinda akajifungua salama mwez wa 7/2013! Lakini ile hali ilizidi kuendelea hata baada ya kujifungua!! Anabanwa pumz, nguvu zinamuishia, moyo unamuenda mbio hata kupelekea kupoteza faham mara kwa mara!! Alikua sometimes anakaa sawa kwa mda mchache kama three weeks ama two kisha inajirudia! Hospital wakawa wanampa bed rest na matibabu kiasi!! Mimi ni mkristo mwenye imani na MUNGU! So nikawa nampeleka hospital na kanisani kufanya maombi! Tumefanya hivyo kwa mda mrefu! Ilibidi niache kaz zangu kipindi ambacho nilitoa (NISHAURI Audio from Am Records) na hata wakat nimepishana na Management yangu ya zamani (Bhits) hata pale wife alikua mgonjwa na studio nilikua sijaenda kwa mda wa miezi mitatu! Nilikua home tu nauguza! kabla ya mapishano kutokea! Na hata ile day nimeenda na wife kwa interview XXL pale pia wife alikua mgonjwa ila alijikaza tu! So kuumwa kwa wife kumefanya nisimame hadi kazi zangu! Ndo maana hata baada ya mapishano btn mm na bhits hamkuendelea kumsikia Mabeste! Niliendelea kuuguza kipindi chote cha 2013 mpaka mwaka jana mwishoni 2014!! Ambapo wife alipata nafuu kwa kiasi ambacho nilidhani yamekwisha sasa naeza rudi kazini! January 2015 nikatangaza kurudi rasmi mzigoni na nikaachia (USIWE BUBU) nilipanga ku fight niachie Usiwe bubu video February, bahati mbaya hali ya wife ikajirudia na ikawa mbaya zaidi ya mwanzo...so ikanibid nitangaze tena rasmi kusimama kazi zangu ili fans wangu msije mkanichukulia vbaya!


PART 2.

Wife wangu kwa sasa ni bado ni mgonjwa sana anahitaji usimamiz wa karibu zaidi haswa kutoka kwangu! Nimempeleka agha khan hosp...akafanyiwa vipimo, wakani hamishia muhimbili kwa ajili ya Ct Scan, ili waangalie kwa ubongo kama una uvimbe au damu imevujia! after CT SCAN ma Dr. Wame suggest apimwe M.R.I kwa vile ana symptoms zote za mtu anayekaribia kupata (STROKE) vile vile imegundulika pia psychological ameshakua affected kutokana na stress za mda mrefu, too much thinking etc. So ameshakua affected hadi imekuja physically anakua anakakamaa mwili! Kiukweli she went through a very hard time kwa kuumwa na mawazo zaidi maana tangu amzae mwanetu Kendrick hajapata malezi ya mama! Vile haezi m take care vizuri wkt yeye anaumwa! Kwa sasa bado Tunaendelea na vipimo na matibabu mpaka atakapo maliza vipimo na kupatiwa matibabu! Tatizo nililo nalo!! Nimekaa home mda mrefu sana miaka miwili na nusu sasa bila kufanya kazi kwa ajili ya kuuguza! Maana hali ya wife nilikua siwez kumuacha na mschana wa kazi au mdogo wangu ambao naishi nao coz hawaezi mhandle wife incase lolote likitokea! Na mda wote huo nimekua niko nae kwa ukaribu sana hata kama natoka issue ya muhim na yy yuko sawa kias basi atajikaza tuta toka wote! Hiii imepelekea Mabeste kutoskika kimziki! Kusimama kwa biashara zangu,kumaliza pesa zangu zote Bank!! Maana ilikua pesa zinatumika bila kuingia! Kwa matibabu na basic needs za daily life! Coz nna wadogo zangu pia nawalea! Hapa nilipofikia naomba msaada wenu ili niweze kumtibia my wife! Coz bado anahitaji kuendelea na matibabu na vipimo! Naamini MUNGU mwema Atamponya lakini kwa sasa Nimekwama kuendeleza matibabu vile for two years na nusu nilikua natumia pesa tu bila kuingiza! So kwa yeyote atakaye guswa Tgo pesa 0715032472 jina la usajiri William V. NGOWI 

Lisa Karl Fickenscher .... Born 1992.......Founder of TEEN TALENTS TANZANIA. .......Talent Manager ->@mabeste_tanzania @ben_d_morestyle .......... Talents : Tv Presenter, Dancer, Genious in marketing idea's & Creative! A loving & faithful wife, A mother of one Child one year and eight months!!!!

Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.