Licha ya kupoteza mchezo wake dhidi ya Nigeria kwenye mchezo wa kufuzu kuelekea michuano ya kombela mataifa 2017,Taifa Stars
wamevuna kitita cha dola 10,000 kutoka kwa Gavana wa jimbo la Akwa Ibom
State,Godswill Akpabio ambapo ndipo unapopatikana Uwanja wa Uyo uliotumika kwenye
mchezo wa jana.
Gavana huyo
alitoa kitita hicho ambacho ni sawa na milioni 21.7 wakati waliokuwa wakipata chakula cha usiku kwa pamoja wachezaji wa Stars baada ya
mchezo huo kutokana na mabadiliko ya kiwango kilichooneshwa na wachezaji wa Stars, ambao walikuwa wakiongozwa na
nahodha wao Mbwana Samatta ambaye kabla ya mchezo huo alikuwa gumzo kwa
Wanigeria ambao wamekua na rekodi ya kifunga Tanzania kwenye michezo yote.
Hata hivyo,wachezaji ambao walionesha kiwango kikubwa sana
kilichowapa mashaka Nigeria ni pamoja na Aishi Manula,
Simon Msuva na mabeki wa kati Vincent Andew na David Mwantika ambapo Gavana huyo pia aliwapa wachezaji wa timu ya Nigeria Naira mil 10 kama pongezi
kwa ushindi wao waliopata na kuahidi kuwapa zaidi endapo watafanikiwa
kupata nafasi ya kushiriki fainali za Kombe la Dunia mwaka 2018 nchini
Russia.
Gavana Godswill Akpabio.