Huenda mali za rapper Nelly zikapigwa mnada kutokana na likimbizo kubwa la kodi linalomkabili ambapo anakadiriwa kudaiwa zaidi ya $2m.
Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ hit maker wa single ya "Dilemma" yupo kwenye mgogoro mkubwa na maafisa wa kodi wanaodai kuwa rapper huyo mzaliwa wa St.Louis amekua akikwepa kulipa kodi huku makadirio ya awali yakionesha anadaiwa kiasi cha $2,412,283.
Hata hivyo maafisa hao wa kodi wanadai kuwa mapema mwaka huu waligundua kuwa tangu mwaka 2013 Mwanamuziki huyo aamekua akifanya mikataba ya kibiashara bila kulipa kodi inayokadiriwa kufikia kiasi cha $149,511.
Kwa muda sasa Nelly hajaachia album mpya tangu ilipotoka album yake ya mwisho "M.O" iliyotoka mwaka 2013 ambapo katika miaka ya hivi karibuni rapper huyo ameelekeza nguvu zake kwenye uandaaji wa vipindi vya Televisheni kupitia kituo cha BET,akiwa miongoni mwa washiriki wa kipindi cha "Reel Husbands of Hollywood" sambamba na kipindi chake cha "Nellyville".