Thursday, September 8, 2016

Huku Mapenzi Yao Yakiendelea Kuwa Gumzo, Hiki Ndicho Rihanna N Darke Wanachoendelea Kukifanya.


Sio kitu cha ajabu tena kuongelea mapenzi ya Rihanna na Drake ambayo yanaendelea kuwa gumzo duniani kote kufuatia wawili hao kuwa na nguvu kubwa ya ushawishi ambayo imewatengenezea mashabiki kibao duniani.

Katika hali isiyo ya kawaida hitsong "One Dance" ya Drake aliyowashirikisha Kyla na Mnigeria WizKid imeendelea kuzikimbiza chati mbalimbali za muziki wa majuu kwa kushika Namba moja kwenye orodha ya ngoma zinazosikilizwa sana kupitia Spotify kipindi hiki cha Summer huko huko marekani.

Drake ameonekana kukimbiza zaidi kwani ukiachana na One Dance kuna ngoma nyingine kama Controlla na Too Good aliyomshirikisha Rihanna zimeshika nafasi ya 2-3n huku namba nne ikimuangukia mrembo Rihanna na ngoma yake "Needed Me"

Kwenye orodha ya Ngoma zinazosikilizwa zaidi Duniani bado "One Dance" ya Drake imeendelea kukimbiza kwenye nafasi ya kwanza ikifuatiwa na "This Is What You Come For" Ya Calvin Harris na Rihanna.


Nyimbo Kumi Bora (Marekani)

1. Drake (feat. Wiz Kid, Kyla) – One Dance
2. Drake (feat. Rihanna) – Too Good
3. Rihanna – Needed Me
4. Calvin Harris (feat. Rihanna) – This Is What You Came For
5. Drake – Controlla
6. Desiigner – Panda
7. The Chainsmokers (feat. Daya) – Don’t Let Me Down
8. Twenty One Pilots – Ride
9. Sia – Cheap Thrills
10. Twenty One Pilots – Heathens

Nyimbo Kumi Bora Duniani.
1. Drake (feat. Wiz Kid, Kyla) – One Dance
2. Calvin Harris (feat. Rihanna) – This Is What You Came For
3. Sia – Cheap Thrills
4. The Chainsmokers (feat. Daya) – Don’t Let Me Down
5. Justin Timberlake – CAN’T STOP THE FEELING
6. Drake (feat. Rihanna) – Too Good
7. Desiigner – Panda
8. Fifth Harmony (feat. Ty Dolla $ign) – Work From Home
9. Mike Posner – I Took A Pill In Ibiza (Seeb Remix)
10. Shawn Mendes – Treat You Better

Kuonekana sana kwa majina yao kwenye Orodha hizo ni dalili tosha kama Albamu zao walizoziachia mapema mwaka huu zinaendelea kuwalipa kutokana na kusikilizwa sana kwa ngoma zao.

Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.