Thursday, September 1, 2016

NEW AUDIO:Chris Brown "What Would You Do".

  Siku moja baada ya mkali wa miondoko ya RnB na Pop,Chris Brown alipokamatwa na polisi kwa tuhuma za kumtishia mtu na silaha na hatimae kuachiwa kwa dhamana ya kiasi cha $ 250,000,Mwanamuziki huyo ameachia wimbo mpya unaofahamika kama "What Would You Do" likiwa ni swali linaloakisi matukio anayoyapitia huku wimbo huu wa kuchezeka ukiwa na mahadhi ya Pop,House na vionyo vya Electro sound.

                                               Chris Brown.

"What do you do? Fighting for your life and no one’s on your side,” ....... “I can’t stand to lose / You see you’re in too deep and don’t know where to hide / I got a question: What do you do".Sehemu ya mashairi ya wimbo huo.


Inadaiwa kuwa Chris Brown yupo kwenye maandalizi ya album yake mpya inayofahamika kama  "Heartbreak on a Full Moon" iliyotanguliwa na video ya wimbo mwingine unaofahamika kama “Grass Ain’t Greener.”

Kuusikiliza wimbo huu bonyeza link hii hapa NEW AUDIO:CHRIS BROWN,"What would you do".

Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.