Kiungo mchezeshaji raia wa Ivory Coast,Yaya Toure ameachwa kwenye kikosi cha Manchester City kitakachoshiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu hii ikiwa ni mara ya pili kwa Kiungo huyo kuwa chini ya kocha Pep Guardiola aliewahi kuwa Manager wake wkati akiitumikia Club ya Barcelona na kupata wakati mgumu kabla ya kuamua kuondoka na kuhamia
Manchester City.
Tayari Guardiola ameshawatoa kwa mkopo wacgezaji kama Joe Hart, Samir Nasri,
Wilfried Bony na Eliaquim Mangala na kuleta mtikisiko kwenye klabu hiyo
yenye maskani yake kwenye dimba la Etihad huku Toure akibakia klabuni hapo baada ya dirisha la usajili kufungwa juzi usiku.
Yaya Toure (kulia) na Kocha Pep Guardiola.
Toure mwenye umri wa miaka 33 alicheza dakika zote tisini kwenye mchezo wa raundi ya
pili wa kufuzu kucheza hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya
Steaua Bucharest, lakini jina lake halijajumuishwa kwenye kikosi hicho
kinachoundwa na wachezaji 21 ambapo Wachezaji wapya kama Claudio Bravo, John Stones, Ilkay Gundogan,
Leroy Sane na Nolito wote wamejumuishwa kwenye kikosi hicho kitapambana na vilabu vya Barcelona, Borussia Monchengladbach na Celtic kwenye Kundi
C.