Mmiliki wa mitandao ya Facebook na Instagram, Mark Zuckerberg.
Huku akiwa ziarani barani Afrika,Bilionea,mmiliki na mwanzilishi wa mtandao wa Facebook Mark Zuckerberge ameonesha kusikitishwa na tukio la hasara ya kiasi cha $200m. mara baada ya kulipuka kwa mtambo wa satelite wa mtandao huo unaofahamika kama "SpaceX Falcom 9" wakati wa majaribio kabla ya kuzinduliwa kwake.
Mtambao huo unaomilikiwa na kampuni inayofahamika kama Elon Musks Co. unadaiwa kulipuka usiku wa tarehe 1 Sept.kabla ya kuzinduliwa kwake wakati ambao Zuckerberg amekua akifanya ziara akizunguka dunia ambapo pamoja na mambo mengine Facebook imepanga kufunga mitambo sita ya satilite ya aina hiyo inayotarajiwa kuzinduliwa Jumamosi ya wikendi hii na kuongeza ufanisi wa mtandao huo kwenye nchi zaidi 14 pamoja na ukanda wa mashiriki ya kati.
Hata hivyo kitengo cha utafiti wa anga nchini humo (NASA) wameunda kampuni binafsi ili kukabiiliana tatizo lolote la kifundi kwenye mtandao huo unaokadiriwa kuwa na zaidi ya watumuaji zaidi ya bilioni 1.49 ulimwenguni.