Kama ulikua huna taarifa,unapaswa kufahamu kuwa kwa sasa Rapper,Jay Z hafanyi tena biashara haramu ya madawa ya kulevya na hii ni baada ya mkongwe huyo wa muziki wa Hip Hop duniani kunaswa na kamera za maaparazi Jijini New York,October 5 mwaka huu akiwa amevaa kofia yenye maandishi yaliyosomeka "Retired Drug Dealer" (Muuza madawa mstaafu).
Rapper huyo ambae ni Baba wa mtoto mmoja,binti Blue Ivy aliezaa na mkewe ambae pia ni Mwanamuziki Beyonc'e Knowles yupo kwenye maandilizi ya kurudi kwenye muziki baada ya kuwa kimya tangu mwaka 2013 alipoachia albamu yake ya mwisho inayofahamika kama "Magna Carta..Holy Grail",ambapo tangu kutoka kwa album hiyo amekua akisikika kwenye colabo za waanamuziki wenzake huku akiwekeza muda muda zaidi kwenye shughuli za kibiashara zilizo chini ya lebo yake ya muziki ya Roc Nation,na huduma yake ya kusikiliza muziki mtandaoni ya Tidal.