Inadaiwa kuwa Mwl.Frank Msigwa alitoa zoezi la somo la kingereza na baadhi ya wanafunzi hawakufanya akiwemo Sebastian.Akiwa darasani mwalimu huyo alimpiga kofi Sebastian ndipo akamhoji kwanini anampiga kabla kukabana na koo na hatimae mwalimu huyo akishirikiana na wenzake walimpeleka ofisini na kuanza kumpiga huku mwalimu aliefahamika kwa jina Ester Harembo kutoka Chuo Kikuu Iringa akiwasihi waache kumshambulia mwanafunzi huyo kwa kipigo bila mafanikio.
Hata hivyo tangu tarehe 29 Septemba mwanafunzi huyo hakuonekana shuleni kutokana na majeraha ambapo walimu hao hawapo tena shuleni hapo kutokana na muda wao wa mafunzo ya vitendo kumalizika.
Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya linamshikilia Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo kwa mahojiano ambapo Waziri Nchemba amegiza kukamatwa kwa walimu hao,huku Waziri wa Elimu,Sayansi na Mafunzo ya Ufundi Prof.Joyce Ndalichako amewafukuza chuo walimu hao na kudai kuwa kwa mujibu wa taratibu za vyuo vikuu walimu hao wametenda kosa la jinai na hawawezi kuendelea na kazi ya ualimu kwakua wamekosa sifa za taaluma hiyo na kuongeza kuwa kitendo kilichofanywa na walimu hao sio cha kufumbiwa macho na jamii.