Friday, October 7, 2016

PICHA:Zaidi ya watu 300 wapoteza maisha nchini Haiti kutokana na Kimbunga Matthew.

Maafisa wa serikali ya Haiti wametoa takwimu mpya kuhusiana na maafa yaliyosababisha na kimbungacha Matthew ambapo inakadiriwa  zaidi ya watu 300 wamepoteza maisha.


Katika Mji wa Jeremie asilimia 80 ya majengo yameporomoka kutokana na kimbuka hicho ambacho kinatajwa kuwa na ukubwa mara nne ukilinganisha na aina nyingine ya vimbuka vilivyowahi kutokea nchini humo huku kikiwa cha  pili kwa ukubwa katika mgawanyo wa aina mbali mbali za vimbunga ambapo kimeelekea katika maeneo mbalimbali ya jimbo la Florida nchini Marekani hali iliyopelekea Rais Barack Obama kutangaza hali ya hatari kwenye Jimbo hilo.


Kimbunga Matthew ambacho ndicho kikubwa zaidi katika visiwa vya Caribbean kwa zaidi ya muongo mmoja uliopita, kimepiga taifa la Bahamas baada ya kupitia Haiti na Cuba.Watu wengi waliopoteza maisha nchini Haiti hasa wale waliokuwa wakiishi mjini na vijiji vinavyojulikana kwa shughuli za uvuvi katika maeneo ya pwani ya kusini mwa Haiti.


Wengi walifariki baada ya kuangukiwa na miti, taka zilizokuwa zikisombwa au hata kusombwa na maji, baada ya mito kujaa maji  kuvunja kingo zao za nyumba kutokana na kuambatana na upepo uliokuwa ukivuma kwa kasi ya hadi kilomita 280 kwa saa.


Usafiri kati ya maeneo ya kusini Magharibi na meneo mengine nchini Haiti ulisitishwa baada ya daraja moja muhimu inayounganisha maeneo hayo kusomba na maji.Mashirika yasiyo ya kiserikali yamesema kwa sasa hakuna huduma za simu na umeme huku mamia ya watu wakikabiliwa na upungufu wa vyakula na maji safi ya kunywa.


 Chanzo;BBC.

Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.