Friday, October 7, 2016

VIDEO:"Sio kampuni yetu wala yeyote bado sijaona kitu,Hip Hop Bongo imelegea"-Lord Eyes.

Former member wa kundi lililowahi kutikisa kunako anga ya muziki wa Hip Hop nchini,Nako 2 Nako,Lord Eyes ambae kwa sasa ni member wa kundi la Weusi,ametoa povu zito ambalo baadhi ya watu wanadai povu hilo ni dongo kwenda kwa members wenzake wa kundi la Weusi.


Lord Eyes ambae akiwa na ndani ya Nako 2 Nako na rapper wenzake,Bu Nako na G- Nako ambae kwa sasa ni sehemu ya Weusi walitamba na hits kadhaa kama "Hawatuwezi","Ndio Zetu","Mpango Mzima","Sweet 16", na nyingine nyingi aliwashangaza mashabiki Jijini Arusha ambapo ndipo ali-perfom hit song ya "Hawatuwezi" na R&B hit maker Baraka Da Prince,kitendo kilichowafanya baadhi ya mashabiki na wadau wa muziki nchini kumshauri rapper huyo kurudi kwenye muziki baada ya kimya kirefu.

"Navyoona kwanza game imelegea,natafuta nyimbo ya kitanzania kuisikiliza  na kuipenda ni-bang nayo,hakuna"....."Sioo kutoka kwenye kampuni yangu sio kwenye mchezo mzima,kote naona legelege,na hicho ndicho kinanifanya nirudi kwa kasi".

Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.