Monday, November 28, 2016

MAMBO 10 YA KIPUMBAVU KUHUSU FEDHA NA MAISHA YETU YA KILA SIKU.

Nadhani wengi wetu tumewahi kusikia ule msemo unaoosema 'mkono mtupu ...haulambwi..!!.Haimanishi mkono wako uwe na mchuzi wa samaki ulioungwa kwa nazi....La hasha,Bali mkononi uwe na fedha.


Hivyo basi kwa kuzingatia changamoto zakimaisha tunazozipitia kila uchwao,haya ni mambo 10 ya kipumbavu yanayotokea miongoni mwa wenye fedha na wasio na fedha.



1.Ukiwa na fedha wapumbavu watakusikiliza kwa sababu ya fedha zako.
2.Ukiwa na fedha wanafiki watakusifu hata kama unawapotosha.Si ajabu hawatakukosoa kwa sababu tu ya nguvu zako kifedha.
3.Ukiwa na fedha mwanamke yeyote mal*ya ni rahisi kumuweka kwenye himaya yako.Hata kama hakupendi kutoka moyoni atakua tayari kuwa na wewe kwa maana ya kukupa mwili wake ili mradi tu apate sehemu ya fedha zako.Si ajabu pia kusikia mwanaume rijali kutekwa kimapenzi na mwanamke kwa sababu ya pesa,kwa lugha ya mjini wanawaita 'mario'.
4.Ukiwa na fedha ni ngumu sana kugundua yupi hasa ni adui yako,kila mtu atajifanya  kuwa rafiki  ila huu ndo wakati ambao maadui wengi huficha sura zao halisi kwa kujifanya kama watu wema kwako.
5.Ukiwa huna fedha usikate tamaa watu wakipuuza au kubeza mawazo yako hata kama yanaweza kuwa na manufaa ya kifedha,ukizipata pengine waliokupuuzia watakua wapumbavu au wanafiki kwako (Rejea point 1 & 2).
6.Ukiwa huna fedha usilalamike watu wasipopokea simu zako au kutojibu kwa wakati meseji unazowatumia,pengine wapo bize wakipokea simu za michongo ya fedha au wakijibu meseji zinazohusu dili za fedha.Hivyo unachotakiwa kufanya ni kuwa mbunifu na kupambana upate fedha.
7.Ukiwa na fedha umri sio kigezo au kipimo cha heshima,si ajabu kijana kuitwa mzee,au mtu akapewa majina ya kumsifu na kumtukuza kama boss,mtu wa watu,tajiri,mshua,doni,trump na mengine mengi.
8.Ukiwa na fedha halafu ukawa mkimya au kutojihusisha kwenye baadhi ya mambo yanayopendwa na wengi,usishangae ukiambiwa kuwa unaringa au unajisikia na kauli nyingine nyingi za kukukejeli.Hiyo ni kawaida,usiisahau uamuzi wa jinsi unavyotaka kuishi ni  wako.
9.Ukiwa na fedha halafu ukawa mtu wa kujisifu mbele za watu si ajabu utaitwa mcheshi ila ukiwa huna fedha ila mzungumzaji si ajabu utaitwa mropokaji.
10.Wengi wakipata fedha hulipa kisasi (mabaya) kwa wale waliowadhihaki wakati wa dhiki,ila kwa mtu mwenye hekima na hofu ya Mungu huwatendea wema hata wale waliowadhiaki na kuwadharau.Kitendo cha aina hiyo huwa funzo kwa anaetendewa na kwa watu wengine kwenye jamii,pia hufanya moyo wa anaetenda kuwa na amani na kutarajia mambo mazuri mbeleni.






Credit; FB-@Mdadisitzrapper   IG-@Mdadisi_therapteaser

Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.