Wednesday, December 14, 2016

MZEE BABA ANASWA AIRPORT AKITOROKA KESI YA KUTISHIA KUMUUA MAMA YAKE MZAZI

Farid Juma (Mzee Baba)
Farid Juma  Janmohammed lakini ye upenda kujiita Fuad Jamal a.k.a Mzee Baba amenaswa  uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere wakati akisubiri Ku kwea pipa la kuelekea uingereza Huku akijua fika kuwa Ana kesi ya kutishia kumuua mama yake mzazi, ina maana alipoona Huku inakaribia machale yakamcheza Akaona bora akimbie 🏃🏃
Ndipo kabla hajafanikiwa kutoroka Maafisa wa jeshi la Polisi nchini wakafanikiwa kumpiga pingu mbele Ya Abiria wenzake
.
Inasemekana eti Mzee baba akaanza Kutokwa na Machozi Kama Mtoto mdogo, 😭😭
.
Mpaka wakati huu Inasemekana Mzee Baba yupo Polisi Kwa ajili ya mahojiano na alipojaribu kuomba dhamana ilishindikana kutokana na Mtuhumiwa huyo kumiliki Passport mbili Za kusafiria moja ikimtambulisha Kama raia wa uingereza na nyingine ikimtambulisha Kama Raia wa Tanzania
.
Inadaiwa kuwa chanzo cha mgogoro Kati ya mtu na mamaake ni masuala ya Nyumba Nyumba ambapo Bi Mkubwa aliingia mkataba Na mwekezaji flan jina kapuni, kwamba Nyumba aliyokuwa anaimiliki ivunjwe Na kujengwa Ghorofa ambalo chini kuna frames halafu juu kuna makazi ya watu, mchongo ukafanyika Mama akapewa baadhi ya Vyumba kwa makubaliano kwamba baada ya Miaka kadhaa Atamiliki Ghorofa lake lote mwenyewe, basi mama akaamua kuwakabidhi wanae Funguo moja moja, sasa inasemekana Farid akaingiwa na tamaa na kutaka apendelewe zaidi Kwa kupewa Nyumba Zaidi ya moja ndani ya Ghorofa Hilo, hivyo  akawa anamlazimisha mama yake Kwa kutishia kumuua kitu ambacho mama yake alikipinga, Ndipo Jamaa huyo akawa anamtishia kumuua na hii si Mara ya kwanza Siku ya Siku Farid alimvamia mama yake akiwa na kundi la wahuni inasemekana kuwa Walitishia kumuua Mama Kama akikataa kwenda sawa na amri yao, Bahati Nzuri majirani na baadhi ya Ndugu waliskia vishindo na makelele ikabidi wakaingilie Kati na kwenda kumuokoa mama yao, mtuhumiwa na wenzake wakachoropoka ikabidi mama akatoe ripoti Polisi ikafunguliwa kesi na kuanza kuunguruma Ndipo Farid alipoona maji yanamfika shingoni Akaona bora atoroke nchi, Polisi walipopata taarifa ndo wakamnasa airport na kumtia ndani.

Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.