Saturday, December 31, 2016

Ufanye Kazi Na Watu Wanaojua Ili Ufikie Malengo - Lizer Classic



Ndoto ya watayarishaji wengi wa muziki hapa Bongo, ni kuona siku moja
wanafanya kazi kwenye studio ambazo wanazimiliki wao wenyewe na
wanaingiza kipato ambacho kitawafaidisha wao mwenyewe bila kupitia kwa
mtu yoyote ambae anawasimamia.


Hali ipo tofauti kwa mkali wa kutengeneza midundo kutokea studio ya
Wasafi inayomilikiwa na Diamond Platnumz, Producer Lizer ambaye mbali na
kuwa na ndoto hiyo,lakini hafikirii kuacha kazi Usafini WCB.



“Inatakiwa unaangalia unafanya kazi vipi, unatakiwa ufanye kazi na
watu ambao tayari wanajua game hii ya muziki inaendaje,ili uweze kufikia
malengo yako,” amesema Lizer.


Lizer ni moja kati ya watayarishaji wa muziki hapa Bongo ambao
wametawala game kwa kutengeneza hits nyingi mwaka huu za wasanii wa WCB
wengine wa nje kama Chege,Jah Prayzah kutoka Zimbabwe.

Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.