Showing posts with label Burudani. Show all posts
Showing posts with label Burudani. Show all posts
Thursday, January 5, 2017
Saturday, December 31, 2016
Ufanye Kazi Na Watu Wanaojua Ili Ufikie Malengo - Lizer Classic
Ndoto ya watayarishaji wengi wa muziki hapa Bongo, ni kuona siku moja
wanafanya kazi kwenye studio ambazo wanazimiliki wao wenyewe na
wanaingiza kipato ambacho kitawafaidisha wao mwenyewe bila kupitia kwa
mtu yoyote ambae anawasimamia.
Hali ipo tofauti kwa mkali wa kutengeneza midundo kutokea studio ya
Wasafi inayomilikiwa na Diamond Platnumz, Producer Lizer ambaye mbali na
kuwa na ndoto hiyo,lakini hafikirii kuacha kazi Usafini WCB.
“Inatakiwa unaangalia unafanya kazi vipi, unatakiwa ufanye kazi na
watu ambao tayari wanajua game hii ya muziki inaendaje,ili uweze kufikia
malengo yako,” amesema Lizer.
Lizer ni moja kati ya watayarishaji wa muziki hapa Bongo ambao
wametawala game kwa kutengeneza hits nyingi mwaka huu za wasanii wa WCB
wengine wa nje kama Chege,Jah Prayzah kutoka Zimbabwe.
Thursday, December 22, 2016
Celline Dion Apiga Chini Dili Hili La Trump
tangu enzi za kampeni nchini marekani wasanii kibao wamekua wakimpinga Rais huyo mpya anaeshika nafasi ya Barrack Obama.
Mtandao wa Us Weekly umeripoti kuwa muimbaji wa hitsong "My Heart Will Go On" Celline Dion ameipiga chini ofa aliyopewa ya kutumbuiza kwenye sherehe za kuapishwa kwa Rais huyo zinazotarajiwa kufanyika January 20, 2017.
Mia - Cava Bien (Official Music Video)
Tuesday, December 20, 2016
Kupitia Biashara Ya Msosi Hivi Ndivyo Shishi Anavuta Mkwanja
Msanii wa Bongo Fleva Shilole ni moja ya wanawake wapambanaji sana kwenye Tasnia ya muziki wa Bongo Fleva kwani mbali na kazi zake za kimuziki lakini pia ni mjasiriamali.
Yapata Mwezi sasa umepita tangia Shilole afungue Mgahawa wake na tayari matunda yanaonekana kwani mrembo huyo kupitia kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio amesema anaingiza faida ya Laki Tano Tsh 500,000/= kwa siku.
“Mimi hata kama waniite mama ntilie ila najua mwisho wa siku naingiza mkwanja wangu sipungukiwi kitu nauza chakula na jioni naingiza laki tano wewe endelea tu kupiga majungu mimi napiga kazi“Amesema Shilole
Friday, December 16, 2016
Ukweli kuhusu Tunda Man kujitoa Tip Top Connection.
Mwanamuziki Tunda Man amefunguka sababu ilinayomfanya asielewane na bosi wake wa lebo ya muziki Tip Top Connection, Babutale.
Akiongea
na EATV kwenye kipindi cha E-News muimbaji huyo singo ya ‘Mama Kijacho’ amesema :
“Najutia kuwa na misunderstanding na bosi wangu. Kiukweli mimi na bosi wangu Babutale hatuko sawa, kosa silijui. Kuna kitu mimi nimemkosea may be au ameamua tu kukasirika na kiukweli hii kuwa mbali na bosi wangu kwenye kazi zangu ninazozifanya nakuwa mwenyewe tu kiukweli it’s pain, naumia.”....“Lakini sometimes mtu anaweza akawa na mwanae akamwambia nenda katafute maisha kivyake japo baba yake anakila kitu, kwahiyo unakuta mtoto anaondoka kutafuta maisha mengine, anabeba zege anafanyaje lakini anajutia kuwa mbali na baba yake. Lakini mimi najutia kwa sababu kazi zangu nakuwa na wakati mgumu wa kuzipush na kusupport kazi zangu lakini Alhamdulillah Mungu anasaidia.”.Alisema Tunda Man.
Hata hivyo alipoulizwa chanzo cha kutoelewana na Boss wake alidai kuwa kuna kipindi alipata dili la kufanya tangazo lakini kuna mtu alimzunguka na nafasi hiyo akapewa msanii mwingine anayesimamiwa na Tale.

Wednesday, December 14, 2016
VIDEO:Baada ya kukutana na Rais Trump,Kanye West kugombea urais 2024.
Baada ya kurudi uraiani ikiwa ni wiki moja tangu alipolazwa hospitali kutokana na maradhi ya msongo wa mawazo,rappper Kanye West amerudi kwenye vichwa vya habari baada ya kukutana na rais mteule wa Marekani Donald Trump.
Kikao baina ya wawili hao kilichofanyika kwenye jengo la Trump Tower,New York City kilitajarajiwa kufanyika hii ikiwa ni baada ya rapper huyo kudai kuwa ingawa hakupiga kura anaamini kura yake ingeenda kwa Trump alieibuka mshindi dhidi ya Hillary Clinton.
"I don’t mean that I don’t think that Black Lives Matter,I don’t mean that I don’t think I believe in women’s rights...because that was the guy I would’ve voted for".Kanye West aliwaambia mashabiki waliohudhuria shoo ya tour yake ya 'Sant Pablo Tour',ambapo hata hivyo aliamua kuikatiza shoo hiyo baada ya kuporomosha dhidi ya vyombo vya habari,watu maarufu akiwemo swahiba wake wa siku nyingi Jay Z.
Ingawa haijawekwa wazi juu kilichojiri kwenye kikao chao,ila Rais Trump kwa kifupi ameeleza kuwa yeye na Kanye ni marafiki wa siku nyingi ambapo kupitia ukurasa wake wa Twitter West amedai amesogeza mbele mipango yake ya kugombea urais wa Marekani hadi 2024 ili kumpa Trump nafasi ya kumsafisihia njia.

Tuesday, December 13, 2016
Rapper Young Thug anavyowakoa Watoto wa mitaani na kuwasaidia watu kupambana na Umasikini
Rapper Young Thung huenda sasa ameanza kukua baada ya kuelezea harakati zake za kurudisha fadhila kwa jamii na kuwasaidia watu kupambana na umasikini ambapo mpaka sasa anawahudumia zaidi ya watoto 10 waliokua wakiishi kwenye mazingira magumu.
Kwenye mahojiano aliyofanya na jarida la PAPER, akiwa na X-Girlfriend wake Jerrika Karlae,memba huyo wa lebo ya 'Cash Money' amedai kuwa anatataka kuwasaidia watoto wa mitaani na kukumbushia simulizi yake ya mtaani wakati alipokua na kati ya miaka 14/15 ambapo alikua akipora watu mitaani kutokana hali ngumu ya maisha.
"I never want my kids to feel like they don't have anything. I had my first child at 14/15, so you can only imagine [what it was like in the beginning]...When you're poor you do anything to survive. You rob and take...Whenever I go back to my side of town — Cleveland Ave [in South Atlanta] — I know I have to bring money, because there will be friends or cousins or people I knew from 6th grade who are going to ask me for money. My fiancée always says I look like Santa Claus, because I'm just giving everyone something".Alisema rapper huyo.
Thug ambae anatajwa kuwa chanzo cha Boss wa wake Birdman kupigana chini na Lil Wayne,kwa mwaka 2016 alifululiza kuachia Mixtape zilizokua na hits kali zilizosumbua kwenye Chati mbalimbali Ulimwenguni kiasi cha staa wa R&B Usher Raymond kuamua kumshirikisha rapper huyo kwenye wimbo wake wa "No Limit".
Monday, December 12, 2016
Mstaa 8 walioushitua Ulimwengu baada ya kukiri kuwa ni waathirika wa Virusi Vya Ukimwi.
Muigizaji Charlie Sheen sio mtu maarufu wa kwanza kukiri haradhani kuwa anaishi na virusi vya Ukimwi ila ni Staa aliefanya uamuzi huo kwenye karibuni baada ya kutamka kwa kinywa chake kuwa ni muathirika wa V.V.U alipofanya mahojiano na kipindi maarufu cha TV nchini Marekani kinachofahamika kama 'TODAY SHOW' mnamo November 17,mwaka 2016.
“I would like to admit that I am in fact HIV – positive,” he told Lauer. “I have to put a stop to this onslaught, this barrage of attacks and of sub-truths and very harmful and mercurial stories that are about me, that threaten the health of so many others and that couldn’t be further from the truth.”.Alisema na kuongeza alifanya makosa mengi hapo awali kwa kuwalipa watu kiasi kikubwa cha fedha ili kumtunzia siri hiyo.
2. Rock Hudson.
Muigizaji Rock Hudson ndiye mtu maarufu wa kwanza kukiri hadharani kuwa anaishi na virusi vya Ukimwi baada ya kufikia uamuzi huo Julai 25 mwaka 1985.
Hata hivyo Hudson alifariki tarehe 2 ya mwezi Oktoba,2016 akiwa na miaka 59,atakumbukwa kwa kuwasaidia watu maarufu wengi kufikia uamuzi huo wa kijasiri wa kukubali hali zao za kiafya.
Taarifa zisizo rasmi zinadai kuwa staa huyo wa Tamthilia maarufu ya 'Pillow Talk' aliambukizwa V.V.U akishiriki mapenzi ya jinsia moja.
3.Earvin ‘Magic’ Johnson.
Staa huyo wa zamani wa klabu ya mpira wa kikapu nchini Marekani ya Los Angeles (LA),alistaafu rasmi 1991 kushiriki ligi ya kikapu huku wakati huo akiwa kwenye kiwango cha hali ya juu na kukiri kuwa alikua ameathirika na Vurusi Vya Ukimwi.
Johnson ambae kwa sasa ana miaka 56 amekua akiendesha kampeni ya elimu kwa jamii juu ya dhana potofu kuwa Ugojwa wa UKIMWI ni ugojwa wa jamii ya watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja.
4.Freddie Mercury.
Kwa mujibu wa swahiba wa Mercury anaefahamika kama Jim Hutton,Mwanamuziki huyo nguli wa miondoko ya R&B na Soul aligundua anaishi na V.V.U mapema kabla ya sherehe za Pasaka mnamo mwaka 1987.ambapo baadhi ya vyombo vya habari vilianza kusambaza tetesi hizo.
Mnamo Novemba 23 mwaka 1993 alitoa andiko rasmi na kuthibitisha kuwa anaishi na virusi vya UKIWMI.
“I wish to confirm that I have been tested HIV positive and have AIDS. I felt it correct to keep this information private to date to protect the privacy of those around me.
“However, the time has come now for my friends and fans around the world to know the truth and I hope that everyone will join with me, my doctors and all those worldwide in the fight against this terrible disease.”.Ilisomeka sehemu ya taarifa hiyo.
Hata hivyo siku moja baada ya kutoka kwa taaarifa hiyo,Mercury alifariki dunia kwa maradhi ya Nimonia hii ikitokana kuwa muathirika wa Virusi Vya Ukimwi.
5.Eazy-E.Mnamo tarehe 24 ya mwezi Februari mwaka 1995,rapper Erick Wright maarufu kama Ezzy- E alilazwa hospitali akiamini kuwa alikua akisumbuliwa na maradhi ya 'Asthama' ambapo baadae ilibanika kuwa alikua ameambukizwa Virusi Vya Ukimwi.
Eazy E ambae alikua memba wa kundi maarufu la HIP-HOP Ulimwenguni la N.W.A (Nig**r With Attitude) alidai kuwa alianza kufanya mapenzi akiwa na umri wa miaka 12 ambapo mpaka anafariki alikua na jumla ya watoto saba na wanawake saba tofauti.
Hata hivyo rapper huyo aliamua kufa na tai shingoni baada ya kugoma kukiri hali yake kiafya hadi taarifa ya maradhi yake kusomwa kwenye mazishi yake baada ya kifo chake mnamo tarehe 26 ya mwezi machi mwaka 1995.
“I just feel that I’ve got thousands and thousands of young fans that have to learn about what’s real when it comes to AIDS. Like the others before me, I would like to turn my own problem into something good that will reach out to all my homeboys and their kin. Because I want to save them before it’s too late,”.Ujumbe huo ulioandikwa na Eazy- E unaodaiwa kuandikwa na mkono wake ulisomwa siku ya mazishi yake na kuwaacha wapenzi wa mmuziki wa Hip Hop nchini Maekani na huzuni kutokana na kifo cha rapper huyo aliefarki akiwa na miaka 30.
6. Arthur Ashe.
Mnamo mwanzoni mwa miaka ya 1980 mcheza tenisi maarufu Arthur Ashe aliaambukizwa Vizuri Vya Ukimwi baada ya kuongezewa damu ya mtu mwenye V.V.U.
Ashe anatajwa kama Mmarekani mwenye asili ya Afrika wa kwanza kushinda taji la ubigwa w michuano ya tenisi la Wembledon na la US Open ambapo alifariki tarehe 6 ya mwezi February 1993.
7.Greg Louganis.
Louganis alibanika kuwa V.V.U mnamo mwaka 1988,ambapo mwaka 1996 mshindi huyo wa medali ya dhahabu ya michuano ya Olimpiki aliiushtua Ulimwengu baada ya kukiri kuwa alikua kishiriki mapenzi ya jinsia moja na kuwa anaishi na V.V.U.
Hata hivyo amekua akishiriki kampeni za kuwasaidia waathirika wa UKIMWI ambapo mwezi Oktoba 2013 alifunga ndoa na mwenza wake Johnny Chaillot.
8.Liberace.
Mcheza Piano huyu maarufu alifariki mnamo mwaka 1987 huku akidaiwa kuwa alifanya siri juu ya hali yake kiafya.
Hata hivyo miezi kadhaa baada ya kifo chake daktari alithibitisha chanzo cha kifo cha Mwanamuziki na kudai kuwa alifariki kutokana na kusumbuliwa na maradhi yatokanayo na UKIMWI.
SASA JIULIZE UNAFIKIRI KIBONGO-BONGO INAWEZA KUTOKEA SIKU MOJA STAA ANAEISHI NA V.V.U AKAKIRI HADHARANI...!? ...THUBUTUUUUUUU......!!!
Sunday, December 11, 2016
EATV AWARDS-2016:HIZI NDIZO FIGISU ZA TUZO YA VANESSA MDEE KUPEWA LADY JAY DEE..!?
Kwa mara ya kwanza kituo cha Televisheni cha EATV kiliandaa na kuratibu utoaji wa tuzo kwa wasanii nchini katika hafla iliyofanyika jumamosi ya tarehe 10 Disemba 2016 kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam,Hii hatua kubwa kwa chombo cha habari kutambua mchango wa sanaa na wasanii ambao kupitia kazi zao vyombo vya habari vimekua vikijozolea wasikillizaji na watazamaji kupitia vipindi vyao hivyo EATV wanastahili pongezi sambamba na kuungwa mkono kwani utoaji wa tuzo sio tu huongeza ari kwa wasnii wetu bali tuzo ni kipimo cha maendeleo ya sanaa kuanzia kwa msanii mwenyewe na sanaa kwa ujumla.Ni aibu mpaka mwaka unaisha tuzo maarufu za Kilimanjaro Music Awards (KTMA),hazijafanyika na wala hakuna taarifa yoyote rasmi ya kutofanyika kwa tuzo hizo,hii ni aibu kubwa sana kwa Baraza la sanaa nchini BASATA ambao ndio waratibu wakuu wa tuzo hizo.
Tuachane na mambo ya BASATA maana nadhani wanachojua ni kuzifungua nyimbo na kuwapiga wasanii faini.Kwa upande wa tuzo za EATV,nawapongeza waandaji kwa ubunifu wao japo tuzo hizo zilitolewa kwa mara ya kwanza.Kila kitu kizuri hakikosi kasoro na tusisahau kasoro zikitazamwa kwa jicho pevu ni sehemu ya kujikosoa,kujitathimini na kuongeza ufanisi,hivyo basi sina tatizo na Ali kiba kuwa kinara wa tuzo hizo kwa kujinyakulia jmla ya tuzo 3 bali nna shaka na ushindi wa Mwanamama,Komando Lady Jay Dee kama mwanamuziki bora wa kike.Sina tatizo na kipaji cha Jide ambae hata mimi ni shabiki wa nyimbo zake ila tukubali tukatae nadhani majaji na waratibu wa tuzo hizi au kwa kujua,kwa kutojua au kwa kusudia wameteleza kwa kutompa Vanessa Mdee tuzo hii hasa ikizingatiwa namna Vanessa Mdee alivyoitangaza nchi yetu kwa nafasi yake kama Mwanamuziki wa kike kutoka Tanzania hadi ubalozi wa Marekani nchini kumchagua Vanessa kuwaongoza mabinti kwenye mdahalo wa kampeni ya elimu kwa watoto wa kike duniani,mdahalo ambao uliongozwa na mke wa Rais wa Marekani,Michelle Obama.
Sitaki niwachoshe na maneno mengi,ila kwa mwaka huu Jide alikua na 'Hit songs' ngapi..? 'Ndi Ndi Ndi','Sawa na Wao' eheee we unaijua nyingine...okey,twende kwa Vanessa,'No Body But Me' aliyofanya na rapper K.O,'Pale kati',bado colabo zake na Navy Kenzo,Mwana Fa,G.K kundi la Weusi bila kusahau colabo yao na X-Boy wake Juma Jux inayofahamika kama 'Juu', hapo hatujazungumzia video yake mpya ya 'Cash Madam' aliyoamua kufunga nayo mwaka.Tusisahau nyimbo zake sio tu zimesumbua kwenye chati za muziki nchini bali hadi kwenye chati za vituo mbalimbali vy kimataifa kama MTV,TRACE MUSIC nk.
Vanessa ametumika na makampuni mangapi mwaka huu kwenye matangazo,kwanini wanamtumia..?,Hata Coke Studio walimpa dili kwa mara ya pili kwenye msimu wa shoo yao ambapo aliungana na mastaa wakubwa ulimwenguni kama Trey Song kutoka nchini Marekani.Tazama FOX Televisheni moja ya vituo vikubwa vya TV ulimwenguni,kila baada ya muda utamuona Vanessa akiwa na kina Patoraking na Casper Nyovest kwenye promo za vipindi vya Afrika,sasa tujiulize kwanini wanamtumia Vanessa,tukubali au tukatae,EATV wamepuyanga kama wanavyosema watoto wa mjini kwa kumnyima tuzo V- Money na kumpa Lady Jay Dee,japo sijajua msingi wa kumpata mshindi ulikua ni kwa kura pekee
Ila ukweli ni kuwa waliotajwa kuwania kipengele hawakua na vigezo vya kumpokonya tuzo hii Vanessa kwa mwaka 2016 kutokana na juhudi zake za kurudisha heshima kwa Wanamuziki wa kike juhudi ambazo hata Komando Jide kwa miongo kadhaa sasa amekua akizifanya kupitia muziki wake.Kama kweli wewe ni mpenzi wa sanaa na unaufatilia muziki unadhani kwa mwaka 2016 Jide,Linner,Ruby na Lilian Mmbabazi kutoka nchini Uganda waliokua wakiwania kipengele cha Mwanamuziki bora wa kike yupi alistahili kupea tuzo hii..?
Hawa ni washindi wa tuzo za EATV AWARDS-2016.
1. Kipengele cha tuzo ya Mwanamuziki Bora wa Kiume 2016 kimekwenda kwa Ali Kiba.
2. Wimbo wa Aje wa Ali Kiba umeshinda tuzo ya Wimbo Bora wa Mwaka 2016.
3. Video ya wimbo wa Aje ya Ali Kiba imeshinda tuzo ya Video Bora ya Mwaka 2016.
4. Kipengele cha tuzo ya Mwanamuziki Bora wa Kike 2016 kimekwenda kwa Lady Jay Dee.
5. Tuzo ya Heshima inayotolewa kwa mtu/taasisi yenye mchango mkubwa katika sanaa ya Tanzania inakwenda kwa Dj Bonny Love.
6. Tuzo ya Filamu Bora ya Mwaka 2016 imekwenda kwa filamu ya Safari ya Gwalu ya Gabo Zigamba.
7. Tuzo ya Mwigizaji Bora wa Kiume 2016 inakwenda kwa mwigizaji Salim Ahmed maarufu Gabo Zigamba.
8. Tuzo ya Mwigizaji Bora wa Kike 2016 inakwenda kwa mwigizaji Chuchu Hans.
9. Navy Kenzo wameshinda tuzo ya Kundi Bora la Muziki 2016.
10. Mwanamuziki Man Fongo ameshinda tuzo ya Mwanamuziki Bora Chipukizi 2016.
J.Cole anavyovunja rekodi zake mwenyewe kupitia album zake bila 'Colabo' na Mwanamuziki yeyote.
Rapper J. Cole huenda akavunja rekodi ya mauzo ya album ya 'Platnum' bila kumshirikisha mwanamuziki yeyote kwa mara ya pili kupitia album yake mpya inayofahamika kama '4 YOUR EYES ONLY' kama alivyofanya awali na album yake ya '2014-FOREST HILL DRIVE'.
Kwa mujibu wa HITS Daily Double, album hiyo mpya yenye jumla ya nyimbo 10 inatabiriwa kufikisha mauzo ya nakala 550,000 hadi 575,000 kwenye wiki yake ya kwanza tangu ilipoingia sokoni ikiifutia album ya rapper Drake inayofahamika kama 'VIWES' ILIYOUZA jumla ya nakala milioni 1.4 na 'LEMONADE' ya Mwanamuziki Beyoncé iliyouza nakala 653,000 kwenye wiki yake ya kwanza.
Takwimu hizi zinamfanya J.Cole kuwa na wiki ya kihistoria kwenye maisha yake ya kimuziki,hii ikiwa ni baada ya album yake ya '2014-FOREST HILL DRIVE' iliyotoka mwaka 2016 kuvunja rekodi ya mauzo ya 'Platnum' mara mbili kwa maana ya kuuza nakala milioni 2 na kufika hadi namba 1 kwenye chati za Billboard 200 ikiwa imeuza jumla ya nakala 371,000.
Album hiyo mpya ya Cole ambayo kabla ya kutoka kwake ilitanguliwa na 'Documentary' aliyoipa jina 'EYES',kwa sasa inashikilia namba 1 kwenye kwenye mauzo ya album kwenye mtandao wa iTune huku singo tatu kutoka kwenye album hiyo,ikiwemo 'Deja Vu',Immortal' na 'Neighbors' zikiwemo kwenye Chati ya nyimbo 20 bora za mtandao huo.
Ni kweli kuwa 'Hakkers' mitandaoni ndio chanzo cha Drake kusitisha kutoa album yake hadi mwaka 2017..?
Rapper Drake amesitisha mpango wake wa kuachia album yake mpya aliyoipa jina 'MORE LIFE' iliyotarajiwa kutoka Disemba 2016,ambapo sasa itaingia sokoni mwaka 2017.
Kupitia Sehemu ya vipindi vya 'OVOSOUND Radio' inayomilikiwa na Drake,Meneja wa rapper huyo mzaliwa wa Toronto,Canada Said El-Khatib alithibitisha uamuzi huo bila kuelezea sababu ya kuahirishwa kutoka kwa album hiyo.
“More Life is coming at the top of 2017,”.Alisema Khatib.
Mwezi Oktoba mwaka huu,Drake kupitia OVOSOUND Radio,aliahidi ujio wa album mpya na kutaja baadhi ya nyombo zilizomo kwenye album hiyo kama 'Two Birds', 'One Stone', ambazo zimetayarishwa na mtayarishaji maarufu wa miondoko ya 'Trap',London On Da Track pamoja na 'Sneakin' aliyowashirikisha 21 Savage na 'Fake Love'.
Thursday, December 8, 2016
HAWA NDIO WASANII 5 BARANI AFRICA WALIOINGIZA KIASI KIKUBWA CHA FEDHA 2016.
Mara nyingi tumezoea kuona list za wasanii wakubwa barani Afrika wakitajwa kumiliki kiasi kikubwa cha fedha.This time around imetoka list inayowataja wasanii watano kutoka Afrika wanaotajwa kuingiza kiasi kikubwa cha fedha mwaka 2016.
5. Diamond Platnumz (Tsh. Bilioni 9,665,923,190.55)
Mtanzania Diamond Platnumz huenda akawa msanii anayezungumzwa au kutajwa sana kwasasa barani Afrika kutokana na headlines anazotengeneza kila siku, mikataba yake na makampuni makubwa kwenye kazi zake pia inazidi kumuweka sehemu nzuri kifedha.
Hakuna shaka kwamba Diamond ni mmoja kati ya wasanii wanaoingiza pesa nyingi kupitia muziki wao kwasasa, na hili litaondoa utata kuhusu kiasi cha pesa alichotajwa kuwanacho staa huyu wa single ya 'Make Me Sing' ambaye aliwahi kuzungumza na E!Television Jumapili ya, June 26 mwaka huu na ikaelezwa kuwa anamiliki pesa zinazozidi kiasi cha dola Milioni Nne za Marekani (Zaidi ya Bilioni 9 za Tanzania).
Kiasi hicho cha pesa hakijaja tu kama suprise kwa Diamond, ambaye anatajwa kuwa ndiye msanii anayelipwa pesa nyingi zaidi kwenye show au event yotote nchini Tanzania na pengine Afrika Mashariki kwasasa.
Pesa nyingi zinaelezwa kuingia kupitia shows alizofanya ndani ya Tanzania, East Africa na nje ya Afrika. Diamond Platnumz pia amekuwa balozi wa makampuni makubwa kama Vodacom, Cocacola, DSTV, Uber Taxi na Red Gold.
Ziko taarifa kuwa Diamond Platnumz huchaji si chini ya shilingi milioni 25 kwa show moja ya kawaida akiwa Tanzania,inadaiwa gharama hizo hupanda mara mbili kwa maana ya shilingi milioni 50 na kuendelea kama akiitwa na kampuni ya biashara na kama akiitwa nje ya Tanzania basi gharama zake huanzia shilingi milioni 200 na kuendelea.
Vyanzo vingine vya mapato ni pamoja na mauzo ya miito ya simu ambayo inaelezwa hakuna msanii yeyote Afrika Mashariki anayefikia mauzo yake kwenye ukanda wa maziwa makuu, pia anamiliki akaunti ya Youtube ambayo ipo kwenye list ya chaneli 10 zinazoangaliwa zaidi barani Afrika.
Hivi karibuni Diamond Platnumz ameingia kwenye biashara za kununua nyumba na kuzifanyia ukarabati ambapo huzipangisha, kitu kinachotajwa kumuingiza mkwanja mrefu zaidi jijini Dar es salaam, mbali na kumiliki record lebel yake ya Wasafi Classic Baby (WCB) ambayo kwa mujibu wake Diamond aliwahi kusema wamesaini deal ya zaidi shilingi Bilioni 1 na lebel ya Universal Music Group ya Marekani ili kusambaza kazi za wasanii walioko chini yake ambao ni Rich Mavoko, Harmonize na Rayvany.
4. Wizkid (Tsh. Bilioni 25,676,809,453.47)
Kwa mujibu wa mtandao wa Infoguide Nigeria, mpaka kufikia December 2015 mwimbaji maarufu kutoka nchini Nigeria,Wizkid alikuwa anakadiriwa kumiliki kiasi cha dola Milioni 11.5 ambazo mpaka mwisho wa mwaka 2016 inaelezwa kuwa amefikisha dola Milioni 12.
Wizkid amekuwa na mikataba inayomuingizia pesa nyingi na makampuni kutoka Nigeria ikiwemo label yake ya Star boy Recordsaliyoianzisha mwaka 2010. Pia mwaka 2014 Wizzy alisaini deal ya kuwa balozi wa kampuni ya simu ya MTN ambao walimlipa zaidi ya shilingi milioni 300 na kampuni ya MTN Rival Globacom ikapanda mara mbili ili kumtumia Wizkid kama balozi wao.
Deal hiyo ya miaka miwili inatajwa kumuingiza Wizkid zaidi ya shilingi milioni 900 kutoka kampuni ya Globacom na mwaka 2015 wakati akifanya sherehe ya kutimiza miaka 25 Wizkid alisaini upya mkataba wake na kampuni ya vinywaji baridi ya Pepsi.
Ukijumlisha kiwango cha pesa anachoingiza kutoa kwenye shows anazofanya, mauzo ya nyimbo zake, tuzo, zawadi pamoja na mikataba yake, inamuweka star huyo kwenye list wasanii wanaoingiza pesa nyingi zaidi nchini Nigeria. Zipo taarifa kuwa ili kuweza kumualika Wizkid aje kufanya show ya kampuni itakubidi umlipe si chini ya shilingi milioni 60.
Kumbuka pia mwezi August, 2015, WizKid alitajwa na jarida la Forbes kama miongoni mwa mastaa 14 wanaoitangaza Afrika kimataifa.
3. Davido (Tsh. Bilioni 30,502,418,406.03)
Kwa mujibu wa mtandao wa Nigerian Finder,Davido anamiliki utajiri unaofikia dola milioni 14 ambazo ni zaidi ya shilingi Bilioni 30 za Kitanzania.
Pamoja na kuzaliwa kwenye familia yenye uwezo mkubwa kifedha, hiyo haikumfanya Davido kurelax badala yake alitumia nafasi yake kama msanii kujenga jina lake na kufanya biashara inayomfanya kuingiza pesa nyingi kwenye akaunti zake.
Mwaka 2012, Davido alisaini deal na kampuni ya MTN TV kama balozi na akasaini deal nyingine na MTN Pulse kuwa muwakilishi wa kampuni hizo kwa kitita cha zaidi ya shilingi milioni 207 za Kitanzania, wakati huo huo mwaka 2014, Davido alilipwa zaidi ya shilingi milioni 341 kuwa balozi wa kampuni ya dawa za meno ya Close UP.
Pia Davido na kaka yake Adewale Adeleke wanamikili lebel ya muziki iitwayo HKN Music ambayo imekuwa ikiwaingiza pesa nyingi kupitia mauzo ya nyimbo za wasanii waliosaini lebel, mauzo ya albam pamoja mikataba ya matangazo.
2. Akothee (Tsh. Bilioni 132,683,540,000.00)
Huenda ukashangaa sana kuona jina la msanii huyu kutokua kubwa sana au kutofahamika sana na watu wengi ila lipo kwenye list hii,Ila ukweli ni kwamba Mwimbaji Akothee kutoka Kenya anatajwa kuwa na utajiri unaofikia dola za Marekani milioni 61 ambazo ni zaidi ya shilingi za Tanzania Bilioni 132.
February 2016, mitandao ya habari nchini Kenya iliripoti kuwa star huyo wa single ya 'Give It To Me' alikuwa anamiliki zaidi ya shilingi za Tanzania Bilioni 8.
Akothee amekuwa akijishughulisha na biashara pamoja na kilimo huku chanzo kingine cha mapato kikitajwa kuwa ni fidia aliyolipwa kama talaka na mwanaume wa kizungu aliyeachana naye miaka kadhaa iliyopita.
1. P-Square (Tsh. Bilioni 277,752,822,639.34)
Wakiwa ni mastaa pekee kutoka Afrika kutajwa na jarida la Forbes mara mbili kwenye list ya wasanii wanaolipwa pesa nyingi zaidi Afrika, Kundi la PSquare limeendelea kuweka rekodi ya kufanya shows za gharama kubwa kupita wasanii wote Afrika, Huku wakipata mialiko kutoka kwa Marais wa nchi zaidi ya 5 na usisahau, mastaa hawa wanamiliki ndege yao binafsi.
Kwa mujibu wa jarida la Forbes, mapacha hao Peter na Paul Okoye,wanamiliki utajiri wa zaidi ya dola za Marekani milioni 130 zinazotokana na mikataba ya kibiashara na makampuni mbambali, biashara za mafuta, mauzo ya muziki na shows wanazofanya.

Credit:E-Daily @Brian Okoth
Wednesday, November 16, 2016
VIDEO:Meek Mill amporomoshea matusi Donald Trump kwenye ''Freestyle'.
Kitifutifu kati ya Wamerekani wenye asili ya Afrika na Rais mpya wa Marekani,Donald Trump kinaendelea kwenye mitandao na vyombo vya habari hii ni mara baada ya rapper Meek Mill kumchana Rais Trump kupitia freestayle kwenye mahojiano na Dj Clue wa kituo cha redio cha Power 105.
“We ain’t grow up like the Jenners / The only choice we had was fuck with yay’ / Sometimes it’d make me wanna run away / Sometimes I see my people struggle and I want to stay. Fuck Donald Trump. Now that Trump won the election. They’re gonna try to box us out like the Mexicans.”
Tangu bilionea Donald Trump alipotangazwa kuwa mshindi wa nafasi ya urais akimshinda aliekua mpinzani wake Hillary Clinton,kumekua na maandamano kwenye baadhi ya majiji makubwa nchini humo na kwenye baadhi ya mataifa wakipinga ushindi wake,hii ikitokana na matammshi na misimamo mikali aliyokua akitoa wakati wa kampeni zake.
Friday, November 11, 2016
Hizi Hapa Salaam Za Shilole Kwa Nuh Mziwanda Saa Chache Baada Ya Kufunga Ndoa.
Jana Novemba 10 mwanamuziki Nuh Mziwanda aliuaga ukapela baada ya kufunga ndoa na mpenzi wake Nawal maarufu Mrs. Mziwanda.
Mastaa mbalimbali wamempongeza Nuh Mziwanda kwa hatua hiyo, Moja kati ya watu ambao wamejitokeza kumpongeza Nuh ni Mama la Mama Shishi Beybe Himself, ambae kupitia ukurasa wake wa Instagram amewapost maharusi hao na kuwasindikiza na ujumbe wa pongezi.
"Hongera Nuh Mwenyezi Mungu awatie Baraka tele kwenye ndoa yenu" Ameandika Shilole..
Ikumbukwe Shilole na Nuh Mziwanda wamewahi kuwa wapenzi wa muda mrefu ambao baadae waliachana na kila mtu kufanya yake.
Kitendo cha Shilole kuwapongeza wanandoa hawa ni dhahiri wazi hakuna beef kati ya zilipendwa hao kama ambavyo Shilawadu na wadau wengine tunavyofikiria...

Wednesday, November 9, 2016
VIDEO:Wema Sepetu kuitambulisha filamu yake na Van Vicker siku ya wapendanao.
Hivi ndivyo mastaa wa muziki wa Hip-Hop Marekani wanavyouchukulia ushindi wa Donald Trump.
Tunaweza kubashiri kuwa raia wengi barani Afrika hawajafurahishwa na ushindi wa Mgombea wa Republican,Donald Trump aliechanguliwa kuwa rais wa taifa hilo lenye ushawishi na nguvu ulimwenguni.Kwa upande wa Wamerakani ambao asili yao si 'Amerika' hasa wenye asili ya Afrika hali mbaya zaidi.
Wengi wao wamekua wakua wakionyesha masikitiko yao kwenye mitandao ya kijamii licha ya Trump kuahidi kuwa atakua Rais wa wote bila kujali waliomchagua na ambao hawakumchagua kwenye hotuba ya ushindi aliyoitoa.
Hizi ni baadhi ya 'Tweet' za mastaa wa muziki wa HIP-HOP ambao wengi wao wamekua wakipinga vikali matamshi tata na misimamo ya yake wakati wa kampeni zake.

Subscribe to:
Posts (Atom)
Comments System
facebook