Dereva huyo ambaye video yake akicheza wimbo wa rapper Darassa huku akiendesha gari ilisambaa mitandaoni.Anadaiwa kufanya kitendo hicho akiendesha gari aina ya
Coaster T360DAY ambalo hufanya safari zake Dodoma kwenda itigi ambapo mashuhuda wa SHILAWADU walipenyeza ubuyu kwa Askari wa kikosi cha usalama barabarani na kufanikishwa kukamatwa kwa dereva huyo.
Dereva huyo anaefahamika kama Said Juma Makachakacha anatarajiwa kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazo mkabili yeye pamoja na wasaidizi wake alikuwa nao kwenye Gari hilo.

