Mwanamuziki muimbaji Rehema Chalamila maarufu kama RayC amekumbwa na tatizo kubwa la kuathirika na madawa ya kulevya. Kwa sasa yumo katika hatua za matibabu ya kujaribu kuondokana na tatizo hilo. Kwa kadri ya maelezo ya mama yake dawa ambazo anahitaji kuzitumia ili kupona ni gharama na pia kama wote tunavyofahamu pia mgonjwa yoyote anatakiwa kula vizuri, mzigo huu ni mkubwa kwa huyu mama, kwa hiyo kunahitajika msaada wa kubeba mzigo huo. Wapenzi wa muziki wa binti huyu na watu wenye mapenzi mema tunaweza kumsaidia mama huyu kwa kumtumia kiasi chochote cha fedha kwa kutumia huduma ya tigo pesa kupitia namba 0655999700Chekanakitime inatanguliza shukrani kwa wote watakao weza kutoa msaada wowote kwa ajili ya matibabu ya mwanamuziki wetu mpendwa.
Source: http://chekanakitime.blogspot.com