Friday, November 11, 2016

Hizi Hapa Salaam Za Shilole Kwa Nuh Mziwanda Saa Chache Baada Ya Kufunga Ndoa.

Jana Novemba 10 mwanamuziki Nuh Mziwanda aliuaga ukapela baada ya kufunga ndoa na mpenzi wake Nawal maarufu Mrs. Mziwanda.
 Mastaa mbalimbali wamempongeza Nuh Mziwanda kwa hatua hiyo, Moja kati ya watu ambao wamejitokeza kumpongeza Nuh ni Mama la Mama Shishi Beybe Himself, ambae kupitia ukurasa wake wa Instagram amewapost maharusi hao na kuwasindikiza na ujumbe wa pongezi.
 "Hongera Nuh Mwenyezi Mungu awatie Baraka tele kwenye ndoa yenu" Ameandika Shilole..

Ikumbukwe Shilole na Nuh Mziwanda wamewahi kuwa wapenzi wa muda mrefu ambao baadae waliachana na kila mtu kufanya yake.
 Kitendo cha Shilole kuwapongeza wanandoa hawa ni dhahiri wazi hakuna beef kati ya zilipendwa hao kama ambavyo Shilawadu na wadau wengine tunavyofikiria...

Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.