VIDEO:Kiwanda cha kutengeneza pombe feki chafumwa Sinza,Dar es salam.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,
Dkt. Hamisi Kigwangalla, ambaye anaongoza timu ya Serikali yenye
wataalamu na wanausalama, kusaka viroba feki na pombe nyingine haramu,
amekamata shehena kubwa ya bidhaa hizo feki kwa maana ya vileo maeneo
mbalimbali ikiwemo kukifuma kiwanda bubu kinachotengeneza konyagi na
'Smirnoff' feki maeneo ya Sinza.
Kiwanda hicho kinatengeneza vinywaji hivyo kwa kutumia 'spirit' ambayo
inachanganywa na 'gongo'; spirit, gongo, chupa tupu na zilizojazwa vileo hivyo,
vizibo, na vifungashio vimekamatwa.
Polisi inawashikilia watu wawili ambao inasemekana wanafanya kazi pamoja
na bwana Yusuf Abdul Kalambo, ambaye anatafutwa na jeshi la Polisi.