Monday, June 7, 2010

RAMA DEE KUPIGA COLLABO NA BLUE 3 KUTOKA UGANDA

Msanii wa R n B hapa Bongo Ramadhani Shaibu a.k.a Rama DEE hivi karibuni anatarajia kusafiri mpaka pande za KAMPALA kwenda kukutana na wakina dada wa Blue 3 na producer wa kundi hilo anayeitwa STEVE JEAN ambapo watapiga mikono miwili ya nguvu.

Katika taarifa yake aliyoituma, Rama DEE amesema kundi la BLUE 3 limemtumia beat ya wimbo wao kwa njia ya Internet ambao hakutaka kuutaja jina lake kwa sababu idea ama wazo linaweza likanakiliwa, katika wimbo huo Rama Dee ameshaandika Mistari, hivyo atakapo tua ndani ya Kampala moja kwa moja ni studio na kupiga mzigo then mengine ndo yatafata.

Katiak mahojiano hayo anasema hajawahi kumchukia msanii yeyote Bongo lakini akamtaja Mkongwe Mmoja wa RnB hapa Bongo ambae kiukweli itakua sio fresh kumtaja.

Amesemaaa jamaa hana uwezo wa kuwa kaka kwenye muziki wa kizazi kipya.

Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.