Monday, June 7, 2010

RAPA RICK ROSS, BUN B KUPERFORM KATIKA BIRTHDAY YA TUPAC


Mwezi uliopita wabongo tulisherehekea siku ya kuzaliwa kwa Bob Marley, safi, lakini hatukusherehekea siku ya kuzaliwa the Natorious B.I.G why? Basi hata hii ya mtu mzima? Tena bado kabisa tarehe zake hazija fika, skia hii

Siku ya Jumatano tarehe 16/06/2010 rapper Rick Ross, Bun B, Too Short, Pill na wengine kibao watakusanyika katika mji wa Atlanta nchini marekani katika Concert ya kusherehekea kuzaliwa kwa Tupac.

Akizungumzia Concert hiyo Bun B amesema amekubali mualiko huo kwani anatambua kwamba ni heshima isiyomithilika kuwepo katika Show hiyo kwani Tupac ni msanii wa aina yake.

Mc wa siku hiyo atakuwa mchekeshaji Mike Epps akishirikiana kwa karibu na mama yake Tupac, Afeni Shakur.

-Pesa zitakazo patikana katika Concert hiyo zitachangia kuendeleza kituo cha sanaa kinachoitwa TUPAC AMARU SHAKUR CENTRE kilichopo pia Atlanta.

Ticket kwa ajili ya kuingia katika Concert hiyo zinauzwa kwa bei ya dola 25 ambazo ni sawa na shilingi za kitanzania 35000/= so kama mkwanja unaruhusu una kwea kitu cha Pipa, unawaambia wakushushe Atlanta TUPAC AMARU SHAKUR CENTRE then pale utajipatia ticket yako mapemaa.

Definately wadau hapa bongo wameshatuskia na tunategemea watashusha bonge la dude la kumuenzi Tupac.


Wakati huo T.I na Eminem wamekutana na kuchagua bonge ya Beat kwa ajili ya wimbo ambao utafanyika baadae na akutupiwa katika album iliyo njiani ya T.I, inasemekana jamaa wamelenga kufanya track ambayo itakua ina Bang ki Club zaidi, pia katika list ya mastaa watakao kuwemo kwenye album T.I King Uncaged mwingine ni Lady Gaga.

Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.