Mwingine akamatwa akihusishwa na mauaji ya Rapa Nussie
Dogo Michael Louding anashitakiwa kwa mauaji ya Rapa wa Louisiana Chris "Nussie" Jackson, aliyeuawa mwezi wa pili mwaka 2009, pamoja na kosa hilo Dogo huyu pia anahusishwa na vifo vingine vitano zaidi.
Chris "Nussie" Jackson aliuawa kwa kupigwa risasi kichwani akiwa nyumbani tarehe 9 mwezi wa pili mwaka jana.
Hapo kabla rapa Lil' Boosie alitajwa na FBI wakimhusisha na kifo hicho na hiyo ni baada shirika hilo kuskia Lil Boosie ali toa dau la dola 30,000/- ili jamaa huyo auwawe.
Kwa wakati huu rapa Lil Boosie anatumikia kifungo cha miaka minne jela.
Dogo Michael Louding anahusishwa na mauaji ya Marcus Thomas, Terry Boyd na mauaji ya Charles Mathews na Darryl Milton yaliyotokea mapema mwezi wa nne mwaka huu.
Mamlaka ya polisi nchini marekani wanategemea kutoa tamko rasmi litakalo elezea zaidi juu ya mashtaka hayo.
Monday, June 7, 2010
Comments System
facebook