Wednesday, July 20, 2011

YOUNG D AZITOSA DOLA ELFU 50 ZA CHOFACO RECORDS

Rapper young kutoka record label ya inayomilikiwa na Mtu mzima Max/ Authentic Studio, amechomoa deal kubwa aliyopewa na Chofaco records yenye makao yake nchini marekani,


Chofaco Records ni Record Label inayomilikiwa na Mtanzania anaitwa Choba Ray anayeishi NCHINI MAREKANI.



Tayari imewahi kufanya kazi na Majina makubwa Industry hii kama King Cassidy, Jeremiah wote wa marekani, lakini kutoka hapa nyumbani studio hiyo imewahi kupiga kazi na Ngosha The Swagger Don, mtu mzima FID Q kwenye ngoma yake inaitwa DANGER FEATURING J . BRYANT



Kwa mujibu wa Young Dee amesema kwamba jamaa wali offer kumpa kiasi cha dola elfu 50 za kimarekani ambazo kwa mkwanja wa kibongo ni kama milioni 75 za kibongo…..na zingetolewa muda mfupi wa baada ya upande wa young Dee kukubali na kudondosha wino kwenye mikataba….



Mpaka sasa utakua unajiuliza ni kwanini Dee alichomoa mchongo huo?



YOUNG D: jamaa ni kweli alinicheki lakini tatizo deal ilikua imekaa ki co operate sana, yani alitaka tumalizane kwa njia ya internet, anitumie mkataba ni using kisha nimtumie makaratasi hayo unyamwezini ndo anitumie hizo pesa dola elfu hamsini,

Inawezekana jamaa hawakua serious sana au walikua serious, ila sisi tukaona tupotezee…



Mitaa flanii: hiyo ndo sababu iliyokufanya upotezee kweli ama kuna sababu nyingine?

YOUNG D: Lakini kuna siku huyo huyo jamaa (Choba Ray) aliwahi kumpigia simu Gols B (Artist/Rapper) akimpa mchongo kama huo mi nakaona design kama jamaa haeleweki, ila milango iko wazi kwa wafanyabiashara ambao watakua wako tayari kupiga na kazi na mimi anytime iwapo.


Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.