Wednesday, September 14, 2016

ROMA: NILISHUHUDIA KIFO CHA BABA YANGU


Msanii wa Hip Hop Tanzania Roma hivi karibuni kupitia mitandao ya kijamii ali share story ya uchungu na kusikitisha juu ya kifo cha baba yake mzazi kilichotokea enzi hizo Roma akiwa mdogo, msanii huyo aliandika maneno haya:-
"Ilikuwa siku ya tarehe kama ya leo 12/9 nakumbuka ilikuwa ni siku ya Alhamisi mida ya saa nne asubuhi....nimebeba chupa ya uji nakuletea hospital
(bombo hospital) Ulikuwa unaumwa sana, nilifika nikakukuta umejilaza kitandani na umezungukwa na mama na bibi na kaka zangu unaongea nao.....ukamiminiwa ule uji na kuunywa vizuri sana......tulikusifia cku hyo kuwa umekula vizuri na ukatupa sana matumaini, dah yale matumaini yalipotea ndani ya dakika 30tu mbele hali ilibadilika Ghafla na ule uji uliokunywa ukaanza kutoka kupitia mdomoni na puani....NILIUMIA SANA NA HIYO PICHA HAINITOKI KICHWANI....kumbe ndio ulikuwa unakata roho, ilikuwa ndiyo kwa mara ya kwanza nashuhudia mtu akifa inavyokuwa, ingawa nilikuwa mdogo lakini nilielewa, niliumia sana mama alipoanza kulia huku akitaja jina lako na kusema usituache usituache....kwakuwa tulikuwa bado watoto tukatolewa nje tusishuhudie lile tukio,
Nakumbuka nikiwa nje nikawa nachungulia kwenye dirisha la kioo huku nalia....hasa nilipoona mama na bibi wanalia, nakumbuka nikaona dokta anakuja kukupima kisha nesi akakufunika shuka mwili mzima hadi usoni....nilizoea kuona hayo mambo kwenye movie tu lakini hapo nilishuhudia mwenyewe na nikaamini kweli ndio umekufa!! Nwayz we all Gud mzee wangu maisha yamebadilika though co kiviiileee still tunapambana....by the way tunamtunza vema mke wako bana hazeeki wala nini!! Ila upweke ulimzidi ikabidi tumtaftie mume wake mwingine bana anaitwa #IVAN @ivanroma2030 kusema kweli tunakuMiss sana baba yetu...na hatuachi kukuombea tukiamini ipo siku tutakutana tena paradiso!! nisikuchoshe baba ngoja nikuache upumzike japo nina story nyingi za kupiga na wewe, nitakucheki wakati mwingine Inshallah!! LOVE YOU DADY....
#GOD_FEEL_ME!! May your soul rest in Peace Baba.

Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.