Thursday, April 5, 2012

AFANDE SELE "TUHUMA ZA VICHUPI NI MATOKEO YA KUTANGAZA NIA YANGU YA KUGOMBEA UBUNGE 2015" CHAMA CHA SIASA CHA C.U.F CHAINUNUA KESI NA KUMNASUA AFANDE MAHABUSU


Afande Sele na Twenty Pa
Katika Ile kesi uliyokua inamhusu Afande Sele, Twenty na wenzao wawili, kwamba walikamatwa na askari wa kituo cha kati cha morogoro baada ya Kufanya vurugu, kujeruhi na kuharibu mali za umma huku wakiwa wamevaa Vichupi(hiyo ni kwa mujibu wa RPC wa Morogoro) tukio hilo lilitokea juzi, jana wakapelekwa mahakamani na kushatakiwa kwa makosa manne, la kwanza Kuwafanyia vurugu karibu na eneo la benk, la pili kuharibu mali ya umma(walivunja kioo cha gari la manispaa) la pili kutembea uchi ni kosa la jinai, na la nne ilikua ni kujeruhi kwa kumkata vidole jamaa flani hivi, makosa yote hayo kila moja lilipangiwa Hakimu wake, na yote walipata dhamana kasoro Kosa la Kujeruhi ambapo waliamriwa waende mahabusu mpaka Majeruhi huyo apate nafuu kwani hali yake ni mbaya sana, Jamaa ikarudi waende mahabusu kwa shingi upande,
Sasa leo naibu katibu mkuu wa C.U.F (Civic United Front) Julius Mtatiro amesema kwamba ilibidi anunue kesi hiyo kwa kuanza kufatilia kila kipengele baada ya kupata taarifa kwamba kesi hiyo ina Mizengwe, Leo majira ya saa sita Mtatiro kwa pamoja na mwanasheria wa CUF wakafanikiwa kuwanasua kina Afande Sele na wenzake, na ikagundulika kuwa huyo majeruhi aliyekua anatajwa haikua kweli kwamba amelazwa hospitali ni mzima na alifika mahakamani jana.
Baada ya kutoka Afande Sele akakanusha kuibuka Town akiwa amevaa kichupi, na kusema kwamba amebambikiwa kesi kwasababu alitangaza nia ya kutaka kugombea ubunge kwa hivyo kuna watu wanataka kumchafua, kwani yeye siku hiyo alienda kuwasaidia ndugu zake walikua wameenda kumkamata mwizi aliyewaibia pikipiki, lakini yeye alipofika kusaidia kumkamata mwizi ndipo askari wanaowalinda wahalifu akiwemo mwizi wao wakawabadilishia kibao Kina Afande na kuwakamata, wananchi walijaribu kuingilia kati ndipo risasi zikalizwa hewani ili kuwatawanya raia.

Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.