Rapper Mabeste
Baadae Sana Hit Maker, Rapper Mabeste kutoka B-Hits studio amefunguka kwamba hivi karibuni amemalizia kupiga picha kwa ajili ya mabango ya Barabarani ya kampuni ya Bia ya TBL kupitia Beer yake ya Kilimanjaro.Mabeste ameishkuru Record Label yake ya B-Hits kwa kuweza kuuvuta mchongo huo, na kuishkuru TBL kwa kumtumia yeye kutangaza biashara yao kwani hawakukosea na soon baada ya Mabango kuwekwa kitaani basi wataona impact yake.
Akifunguka kuhusiana na thamani ya Deal hiyo Mabeste amesema ni zaidi ya milioni kumi, na hawezi kuzitumia vibaya fedha hizo ama kupagawa na wingi wake kwani design kama amezoea hivi, kwani anakumbuka wakati akiwa na umri wa miaka 18 aliwahi kumiliki milioni 20 alizokua amerithishwa na marehem mama yake R.I.P so 10 m sio ishu,
Story kwa hisani ya "You Heard" ya XXL/Clouds fm