R.I.P Steven Charles Kanumba (8/01/1984- 7/04/2012)
TUKIO LILIVYOKUA JANA USIKU:
Mida ya Saa Sita
usiku, Steven Kanumba akiwa
na Mpenzi wake wa siri (LULU) alitoka Chumbani na kwenda kuoga ili aingie viwanja, alipomaliza
wakati anarudi chumbani akamskia mpenzi wake kwa mbali anaongea na simu,
kufungua mlango akamuuliza unaongea na nani mida hii? Akajibiwa kuwa kuna
Kampuni inataka kumpa deal ya Movie, lakini yeye Kanumba katika hali ya kawaida
akaona haiwezekani saa sita za ucku watu wapeane deal, wakaanza kujibizana, huku
Kanumba akimshushia Kichapo Lulu, ndipo huku na huku mwanadada akaona ajitetee,
mwisho wa siku Kanumba akasukumwa na kuangukia kisogo na kuwa Kiiiiiimya, Lulu
ndo akashtuka na kwenda kumwita mdogo wake Kanumba ambaye alikua chumba
kingine, dogo kufika na kuona hali ya Bro, ikabidi atoke Nje kufanya ustaarabu
wa kumtafuta Daktari ili aje kuokoa maisha ya Kanumba na vile vile kuwashtua
ndugu na jamaa, ndipo Lulu akapagawa na kupata upenyo wa kutoroka eneo la Tukio,
watu kufika Kanumba alishakuwa wa baridi cku nyiiiiingi, ikabidi utaratibu wa
kuupeleka mwili wa marehemu hospitali ya Taifa Muhimbili ukafanyika.
BAADA YA MWILI WA KANUMBA KUPELEKWA MOCHWARI:
Saa nane za usiku,
ndipo baadhi ya wasanii wakaanza kujadili yuko wapi aliyesababisha Kifo hicho?
(LULU) wakatoa taarifa polisi sasa kumbe kuna kijana anaitwa Junior miongoni
mwa kundi hilo, akaziskia taarifa hizo, na baada ya muda mfupi kwa siri akampigia
simu Lulu kuwa wakutane mahali, anataka ampatie mkanda mzima, basi wakapanga na
kukutana maeneo flani kwa siri.
LULU ALIVYOKAMATWA:
Inasemekana Polisi
walifanikiwa kuwakuta kwa pamoja, ndipo waigizaji wakashtuka, Duh!! Huyu si
tulikua naye huyu?
Lulu alikutwa akiwa
naked(bila Nguo) huku akiwa amepagawa, Yes of coz lazma awe amepagawa katika
hali kama hiyo, lakini pia alikutwa ameumizwa vibaya usoni, (hiyo ina maana
kuwa walipigana na Kanumba)
Sijataja mahali
walipokutwa na baadhi ya majina kwa sababu za kiusalama, coz bado upelelezi wa
polisi haujakamilika.
KUTOKANA NA KOSA LA KUUA BILA KUKUSUDIA, LULU
KUHUKUMIWA ZAIDI YA MIAKA MIWILI JELA:
Endapo muigizaji wa
Kike Lulu Michael atakutwa na hatia pindi atakapo pelekwa mahakamani basi
huenda akahumiwa kuanzia miaka miwili na kuendelea, kama ilivyotokea kwa
Daktari wa Michael Jackson (Dr Conrad Murray) nchini marekani,
Ila kesi yake
inaweza kuwa ndefu zaidi kutokana na yeye Lulu kutoroka eneo la tukio muda
mfupi tu baada ya Kanumba kufa.
IMEANDIKWA NA MSOMAJI WA BLOG JINA KAPUNI
IMEANDIKWA NA MSOMAJI WA BLOG JINA KAPUNI