Mwigizaji wa Bongo Movie ambaye kwa kipindi kirefu amekua akitangazwa kuwa anaumwa, hadi kupelekea kusafirishwa kwenda INDIA kwa ajili ya matibabu, weekend iliyopita yani jana zilisambazwa taarifa za kizushi kuwa ameaga dunia, lakini huku na huku kupitia Movie Leo ya Clouds fm, Msanii huyo amefunguka kuwa yupo hai fit kama Rambo (Rambo- muigizaji wa movie za Action Hollywood) na anaendelea kuongoza filam itakayotoka hivi karibuni, Sajuki amefunguka kuwa ni kweli anaumwa sana lakini hana budi kuendelea ku shoot ili aweze kupata hela ya kugharamia matibabu, kwani atatakiwa kurudi hospitali ya India hivi karibuni. akamalizia kwa kusema, "waliozusha nimekufa ni watu na chuki zao (haters) wasionitakia mema, wanataka watu waliojitolea kunichangia pesa za matibabu wasinisaidie"
Skiza mahojiano ya Sajuki na mtangazaji KIMODO wa Leo Tena ya Clouds fm, hapo chini