Thursday, May 27, 2010

Mcheza Filamu wa Hollywood ajumuishwa kwenye filamu mpya ya 50 Cents


Mcheza sinema maarufu duniani Ray Liotta amejiunga kwenye project ya movie mpya ya 50 Cent inayoitwa Things fall apart.
Ray Liotta ni mcheza sinema kutoka Hollywood ambae amewahi kuigiza filamu nyingi maarufu kama Good Fellas na Blow, katika movie hiyo Liotta ataigiza kama daktari.
Script ya movie Things fall apart imeandikwa na 50 Cent kwa kushirikiana na Brian Miller na itatengenezwa na kusimamiwa na Kampuni ya Fiftty inayoitwa Cheetah Vision Films.
Filamu hiyo inamhusu mchezaji wa Football ambae anakuja kugundua kuwa ana Ugonjwa wa Cancer katika mwaka wake wa Mwisho chuoni.
Kwa mujibu wa producer wa filamu hiyo anasema imebidi 50 Cent apungue uzito wa Paundi 60 ili aweze kuigiza nafasi hiyo.
Things Fall apart, imeigiziwa katika mji wa Michigan, na Director wa filamu hiyo ni Mario Van Peebles, mastaa wengine katika filamu hiyo ni Lynn Whitefield, Steve Eastin na wengine kibao kutoka Hollywood.
Rick Ross aibuka na kumpeleka mahakamani Rapper Rick Ross
Hivi unamjua Rick Ross? Wengi wenu mnaweza mkahisi namzungumzia William Leonard Roberts II a.k.a Rick Ross anayetamba kwenye ulimwengu wa Hip Hop, simaanishi huyo namzungumzia muuza madawa ya kulevya aliyewahi kuvuma miaka ya 1980 nchini marekani.
Jamaa baada ya kunusurika na kifungo cha maisha na kutoka jela mwaka 2006 hiyo ni baada ya kutumikia miaka 10 ndani amelalamika kuwa rapper
William Leonard Roberts II a.k.a Rick Ross aliingia mkataba wa mamilioni ya dola mwaka 2006 ili kuonesha taswira ya Rick Ross muuza madawa katika filamu.
Rick ross amedai kwamba mwaka 2006 aliwahi kuiandikia barua ya Onyo kampuni ya Defjam ambayo ndiyo inayosimamia kazi za rapa Rick Ross lakini lebo hiyo ilipuuza madai yake.
Vyanzo vya habari vinadai katika kesi hiyo rick ross wa ukweli anadai kuwa jamaa ameibiwa Identity yake na tabia yake ya muuza madawa ya kulevya katika jamii ya watu weusi.
Katika kesi hiyo Rick Ross amepanga kuwafikisha mahakamani makampuni ya Def Jam, Universal, Rapper Rick Ross na Wengine.
Wakati huo huo Rapper Rick Ross anapanga kurelease album yake Telfon Don. hivi karibuni.
Rick Ross na Rick Ross Rapper kiukweli image zao ama Taswira zao zina fanana sana.

Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.