Chameleone kwa Stage |
Dr Jose Chameleone kutoka Uganda weekend hii alipiga bonge la show (Badilisha Concert) na kudhihirisha kuwa msanii kukubalika ni wakati wote muradi tu awe anaendelea kufanya vizuri kimuziki, tofauti na imani tulizonazo wabongo wengi pale tunaposemaga kuwa eti "flani tyme yake ishapita" Chameleone aliperform katika nyomi la watu zaidi ya elfu 20, huku akiwa amepanda kwa stage na zile nguo za kina Armstrong ( mwanadamu wa kwanza kutua mwezini) jamaa alisindikizwa na wasanii wenzake wakubwa afrika mashariki kama Profesa Jay na Red San kutoka Nairobi Kenya