Monday, May 27, 2013

YOU HEARD : MFANYAKAZI WA HOTELI ADAI MESEN SELEKTA AYEYUKA NA DENI LA LAKI 3

Producer Mesen Selekta
Mwanadada mmoja mfanyakazi wa lodge flani jijini mwanza, amejitokeza na kutiririka kuwa eti Producer Mesen Selekta mwezi mmoja uliopita alitoroka katika hoteli yao huku akiwa na deni la zaidi ya shilingi laki tatu, dada huyo amedai kuwa bosi wao ana mpango wa kuwakata mshahara mwanadada huyo na mwenzake kwa uzembe walioufanya kwa kumkubalia mgeni huyo kabla hajalipa mkwanja wowote, mwanadada huyo amedai kuwa walikubali kumpangisha mteja wao bila malipo kwasababu walijua ni mtu mashuhuri basi hawezi kuwa tapeli, inasemekana kwamba mteja huyo aliishi kwenye hoteli hiyo kwa zaidi ya wiki tatu ndio maana bili ikawa kubwa, nilipomuuliza ana uhakika gani kama mtu huyo ndo Producer Mesen akajibu kuwa ndivyo alivyo andikisha kuwa anaitwa Gelly Katoto a.k.a Mesen Selekta, muhariri nilipojaribu kumcheki Mesen kwa bahati mbaya hakupokea simu yake.
skiza mwanadada huyo akitiririka hapo chini ndani ya You Heard:


Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.