Jana asubuhi jiji la arusha lilipata mshtuko mkubwa na simanzi nzito baada ya kutokea kwamlipuko wa mabomu uliotokea katika kanisa la kikatoliki huko olasisti nakupelekea vifo na majeruhi kwa baadhi ya waumini waliohudhuria katika sherehe ya ufunhuzi wa kanisa..
CHANZO..
Haya nimaelezo ya kijana aliyedai kuwa alishuhudia tukio hilo.
Kijana huyo(chini pichani aliyevalia tisheti ya njano) ametueleza kwamba
bomu hilo lilirushwa na kijana mmoja ambaye kimwonekano alikuwa
nikijana wa miaka 20-25. alizidi kueleza kwamba baada ya kijana huyo
kurusha bomu alikimbia huku akiita MWIZI MWIZI MWIZI..
Eneo bomu lilipoangukia likiwa limezungushiwa utepe na jeshi la polisi |
Baadhi ya mejeruhi |
Raia wakiwa wamejikusanya eneo la tukio |
KUKAMATWA KWA MTUHUMIWA..
Kwabahati nzuri tulipata maelezo kutoka kwakijana ambaye alishirikiana
na wananchi wengine kumkimbiza mtuhumiwa kutoka olasiti hadi katika
kijiji kiitwacho ndorobo.. kijana huyo(mtizame mwisho kabisa katika post
hii) alizidi kutueleza ya kuwa mtuhumiwa alikimbia kisha alijilaza
katika miwa ila walisaidia na mbwa waliokuwa wakimkimbiza mtuhumiwa
huyo.. mara baada ya kumkamata walimkuta akiwa na mfuko wenye bomu
zilizobakia.. dakika chache wananchi wenye hasira kali walifika eneo
alipokamatiwa mtuhumiwa huyo wakiwa na silaha kali za jadi wakitaka
kumuua kijana huyo ndipo polisi waliokuwa wakisaidia na wananchi hao
walifika eneo lile nakumchukua mtuhumiwa huyo..
Posted by : David Mollel on :Sunday, May 5, 2013
http://nyumbayahabari.blogspot.com
http://nyumbayahabari.blogspot.com