Sunday, May 5, 2013

KILICHOMSIBU MFANYA BIASHARA HUYU MPAKA KUJIRUSHA GHOROFANI NI NINI?

Maskini weeeee, mfanyabiashara aliyejirusha kutoka ghorofani akiwa amelazwa pembeni ya barabara tayari kwa ajili ya kuwahishwa hospitali kwa matibabu
Mfanyabiashara katika moja ya Maduka ya Kariakoo dsm, amejirusha toka ghorofa ya 9 ya Hoteli ya Concord iliopo Maeneo ya Kariakoo jijini Dar es Salaam na amekimbizwa hospitali kwa uangalizi zaidi maana haijafahamika kama kapoteza Maisha au bado yu hai.
Mfanyabiashara huyo alijirusha toka ghorofani na kuangkia katika Gari aina ya Toyota Corolla ambayo ni taxi iliyokuwa imepaki nje ya hoteli hiyo,chanzo cha kujirusha kwa mfanyabiashara huyo bado hakijafahamika mpaka sasa.

Mashuhuda wa tukio hilo lililotokea muda mfupi uliopita,wanaeleza kuwa walipatwa na mshtuko baada ya kusikika kishindo cha kitu kilichokuwa kimeangukia gari hilo na waliposogea kushuhudia ndipo walipobaini kuwa alikuwa ni mtu huyo alietambulika kwa jina moja la Shirima.
Kwa hisani ya www.thisisdiamond.com

Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.