Kufuatia
mlipuko wa bomu uliotokea tarehe 4 mwezi wa tano katika kanisa la kikatoliki
huko olasisti nakupelekea vifo na majeruhi kwa baadhi ya waumini waliohudhuria
katika sherehe ya ufunguzi wa kanisa hilo, zikawepo rumors kuwa eti
mlipuko huo unahusiana na tofauti za kidini, sasa weusi kampuni, inayoundwa na
baadhi ya wasanii wenye nguvu kutoka arusha, hapo nawazungumzia kina joh
makini, g nako, bonta, lord eyez, na nikki wa pili
wametoa waraka.
Usome hapo chini
Nafahamika kama Nicksson Simon ama Niki wa Pili mzawa na nimekulia Arusha, kuhusiana na suala ambalo limetokea Arusha kwanza kama Weusi Kampuni / wakazi Arusha tunatoa pole sana kwa watu ambao wameathirika na hilo janga, wale ambao wamepoteza maisha mungu awalaze mahali pema peponi, na wamepoteza maisha katika harakati ya kutetea uhuru wao na nchi yao.
Sisi Tamko letu ni kwamba WEUSI tumeliangalia hili suala kwa kina na tumegundua yafuatayo:-
- Tanzania hakuna udini, kwa sababu watanzania wote tumesoma shule moja, tunaishi pamoja tunashirikiana, tunaowana, tunashiriki maulidi, wakristo tushaalikwa futari so tunakula futari, tunashiriki harusi tunashiriki harusi tunashiriki sherehe.
Ili kuweza kuelewa hili tatizo vizuri tuangalie na ulimwengu sasa hivi uko wapi? umetoka wapi na nini kinaendelea.
Moja kati ya majeruhi wa bomu la Arusha |
tunaona uvunaji unaendelea Nigeria, Congo, Sudan, mpaka sasa hivi takwimu zinaonyesha wa Congo milioni 5 washapoteza maisha, wa Sudan takriban watu laki 3 washapoteza maisha, hili tukio linatokea Tanzania leo hii kwa sababu leo hii Tanzania kuna uvumbuzi mkubwa umetokea kuna Uranium, gesi na mafuta kwa hiyo Theory ni ile ile kama ilivyofanyika nchi nyingine inaletwa Tanzania, sasa tunaletewa Adui wa bandia, haya machafuko yanaweza kuja kwa picha nyingi, unaweza ukaletewa kwa picha ya Udini, harakati, maandamano, watu wanakaa ni wasomi inaitwa conspiracy Theaory,
watu wasomi wanakuja katika nyanja mbalimbali lakini lengo ni kuchukua rasilimali na kutengeneza vita au machafuko katika eneo ambalo rasilimali zinapatikana, kwa hiyo watanzania wanatakiwa waelewe kitu kimoja tu huu udini unaosemwa ni adui wa bandia anatengenezwa, kinachotakikana haswa ama tatizo ni rasilimali zinatakiwa zichukuliwe na nchi kama Tanzania inaonekana kwamba ukiruhusu ikatumia rasilimali zake vizuri ndani ya miaka 20 au 25 inaweza ikawa kama........................................
MALIZIA KUSKIZA WARAKA HUU KWA KUSKIZA SAUTI HIYO HAPO CHINI: