Tuesday, May 7, 2013

YOU HEARD : AMAZON ANADAIWA NA MUUZA MA BEGI



Muuza mabegi aliyejitambulisha kwa jina la Melecky Kalonga ameliambia gazeti la makorokocho kuwa anamdai begi msanii wa bongo flava anayefahamika kama AMAZON / CHECHE RHUMBA, Melecky amedai kuwa alifatwa na Amazon na akaombwa amuazime begi kwa madai kwamba anaenda kushoot music video na atakapomaliza tu Amazon atalirudisha, sasa ule muda walio pangiana umepita na Amazon haja rudisha begi la watu mpaka leo na akipigiwa simu hapokei, hivyo ameamua kufungua file polisi na akimkamata mtuhumiwa wake atampeleka mbele ya sheria la sivyo basi arudishiwe begi au pesa shilingi elfu 60, kwani ndio thamani halisi ya begi hilo. 
Akizungumzia shutuma hizi AMAZON amesema kuwa ni kweli aliazima Begi kwa muuza mabegi huyo mwenye goli lake pande za mwenge, lakini video mpaka leo hajamaliza, kutokana na mvua kunyesha mara kwa mara jijini Dar es salaam.
WASKIZE WOTE WAKITIRIRIKA NDANI YOU HEARD YA XXL/ CLOUDS FM:





Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.