|
JUMA NATURE |
|
mfano wa kanda mbili za HALISI |
Zikiwa zimepita wiki kadhaa tangu msanii mkubwa wa bongo flava Juma Nature atolewe nduki kwenye tv station flani hapa bongo hiyo ni baada ya kudaiwa kwenda mahojiano ya TV live huku akiwa amevaa kandambili , msanii huyo ameamua kuja na kanda mbili zenye brand yake, na zitakua zinaitwa HALISI, akatiririka kuwa kwa sababu kila mtu bongo lazima atumie kanda mbili, kwa hiyo kanda mbili ni kitu muhimu katika maisha ya watu masikini na wasio masikini, alipoulizwa na muhariri wa gazeti la makorokocho kwanini katika kikao flani cha maamuzi alikataa zisiitwe NDALA ZA JUMA NATURE? akajibu kuwa akitumia jina lake itakua haijakaa sawa, ila akitumia HALISI ni neno linalojumuisha wote