Mama Sharomilionea |
Mama Sharo ametiririka kuwa kuna Gari aina ya Oper, ambayo alikubaliana na Mudy Suma rafiki wa Marehemu Sharo kwamba iuzwe halafu yeye wampelekee Pesa bado hajapewa wala kuambiwa chochote, pia kuna Pesa za Pango la nyumba aliyokua ameikodisha sharo milionea, kwa sababu sharo alihamia katika nyumba hiyo na kuishi kwa muda mfupi ndo akafariki dunia,
Nilipomuuliza kuhusu Bajaj ya iliyooachwa na Sharo, mama alijibu kuwa Bajaj hiyo inafanya kazi ya kubeba abiria jijini na Pesa za biashara hiyo amekua akitumiwa karibu kila wiki na kijana aliyekabidhiwa kuiendesha.
Mama Sharo aliongeza kuwa anaomba wahusika wampe haraka Pesa hizo ili akajenge nyumba kwenye kiwanja kilichoachwa na marehem maeneo ya Mbezi kwa sababu akichelewa chelewa watu watakimega kiwanja au kukidhulumu kabisa.
Licha ya mali zilizotajwa hapo juu, pia kuna movie aliyoigiza Sharomilionea na Kitale hajaambiwa imeishia wapi japo bado haijaingia mtaani.
Lawama zote hizi ameangushiwa Muddy Suma, jamaa ambaye gari yake aina ya Harrier ndiyo aliyopata nayo ajali Sharomilionea na kusababisha kifo chake, na walikua wamebadilisha na gari yani Sharo alimwachia Muddy Gari yake aina Oper, ila Muddy Suma aliahidi atalirudisha gari hilo kwa wazazi wa Sharo na yeye amesamehe kiroho safy.
Msikize mama Sharo alipokua anaongea na XXL ya @cloudsfm