Inafahamika wazi kuwa Ngoma ya Quick Rocka aliyomshirikisha marehem Albert Mangwea pamoja na Shaa "My Baby" beat na Ryhtm yake zinafanana pasi na shaka na wimbo wa Msanii mkongwe wa Bongo Flava Dully Sykes kwa asilimia Nyingi, nauzungumzia wimbo wa Dhahabu ulitoka zaidi ya miaka 6 iliyopita, sio kesi, lakini hapo kati inavyoonekana hakukua na mawasiliano (miscommunication) kati ya wasanii hao wawili, swali je kwanini nimejiamini kusema hivyo? jibu Simple tu baada ya kuskiza jibu alilotoa Quick Rocka baada ya kupigwa swali na mtangazaji wa kipindi cha XXL ya Clouds fm, kwamba kuna mfanano kati ya ngoma yake na Ngoma ya Dully Sykes, hivi ndivyo alivyojibu "wakati tunafanya hiyo ngoma mimi tayari nilikua na Idea zangu nikampelekea Producer Maneke, tukapiga midundo tukamaliza,, tukaanza kuskiliza ndo tukashtukia Progression ya Dundo inafanana na Dhahabu, ndo nikamskilizisha Boss wangu (Master Jay) naye akasema hivyo hivyo, nikamuuliza sasa tunafanyaje? akanijibu sio mbaya ni kitu cha kawaida tu kwasababu hata hiyo Dhahabu yenyewe imerekodiwa MJ RECORDS" mwisho wa kunukuu.
Sasa kutokana na kauli hiyo katika hali ya kawaida tu jamaa ilibidi amcheki Dully japo kumwambia tu, coz Daressalaam sio kubwa, kutoka Mbezi mpaka Tabata kwa Kina Dully sio mbali au tufanye jamaa yuko busy, vipi kuhusu namba ya simu hana? kwasababu anapoichukulia poa poa ishu hiyo