Monday, August 12, 2013

VIDEO: WALTER CHILAMBO AKANUSHA KUDHULUMIWA KITITA CHA SHILINGI MILIONI 50 NA BSS, AFUNGUKA KUWA YEYE SI MCHOVU KAMA ALIVYODAI NEY WA MITEGO

 
Mshindi wa Bongo Star Search 2012 Walter Chilambo leo ndani ya kipindi cha XXL ya Clouds fm amefunguka jinsi alivyojiskia baada ya kuiskia ngoma ya Rapper Nay wa Mitego inayoitwa Salam Zao, ambapo ndani ya ngoma hiyo Nay alidai muandaaji wa shindano la Bss Madam Rita hajatoa kitita cha shilingi milioni 50 zilizo tangazwa kutolewa kwa mshindi wa mashindano hayo ambayo kipindi chake cha Tv kina mashabiki wengi nchi nzima. Mistari ya Nay katika Ngoma Yake inasema:-
Hizi salam ziende kwa Madam Rita na Bongo Star search,
mshindi analipwa nini mbona kama maguashi,
namwona Walter Chilambo kapigika kama Zamani,
Haji Ramadhani kachoka yuko Kitaani,
milioni Hamsini zao anazila Nani?
Acheni ubabaishaji wekeni mambo Hadharani,
na kwenye Outro Nay Wa Mitego anamaliza kwa kusema Walter Chilambo Niaje Mwanangu, Najua Una hali mbaya Kiuchumi, milioni hamsini Huna Hata Baiskeli? Huna wewe hizo mfikishie salam Madam Rita mwambie sina tatizo nae,
sasa akijibu Madai ya Nay wa Mitego, Walter Chilambo ametiririka kuwa kwake yeye ni Faraja, kwasababu yeye ni msanii mpya na kutajwa na msanii mkubwa kama Nay ni vizury kwa sababu inatengeneza attention kwake yeye Chilambo, na kuhusu milioni 50, Chilambo anasema amepewa zote bila utata, na kuhusu Kutokumiliki vitu vya thamani, akasema kwamba hawezi kutangaza ana miliki mali gani, ila yuko fiti kiuchumi na anaishi anavyotaka yeye kwa ushauri wa wazazi na baraka za mungu.





Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.