Miongoni mwa mastar wa Tanzania wenye ushawishi mkubwa ni pamoja na
Wema Sepetu ambaye pia aliwahi kuwa Miss Tanzania 2006 ambaye kwa sasa
anaendesha kampuni yake binafsi iitwayo Endless Fame inayojishughulisha
zaidi na utengenezaji wa Filamu mbalimbali.
Kupitia kipindi cha Leo tena February 28 Wema Sepetu amekubali kutaja
sifa za mwanaume anayempenda kuwa na mvuto kwake,swali lililoulizwa na
Watangazaji wa kipindi hicho ni kuhusu mwanaume wa sifa gani anayedhani
anaweza kuolewa nae ambapo Wema alijibu>>’Kuolewa sio shida je
huyo mwanaume nampenda,maana naweza kuja kuchumbiwa lakini nisimpende’
‘Mimi nampenda Mwanaume mweusi,wanaume weupe sio kwamba sijawahi kuwa nao lakini nakuwa sina mzuka nao’.
Alipoulizwa kuhusu uhusiano wake na Diamond amekiri kwa
kusema>>’Kweli niko na Nasib[Diamond] na nadhani muda huu kutakua
na utulivu ndani yake,ule utoto tuliokua tunafanya nadhani ulikua utoto
na imekua Power Couple toka mwaka 2010 kwa hiyo tuna ni miaka 4 sasa,kwa
sasa tumeamua kuwa serious’.
Wema Sepetu pia kaandamana na Ant Ezekiel kwenye interview ya kipindi hicho kinachorushwa na Clouds Fm.
Habari kwa Hisani ya Millard Ayo.Com