Inspektah Haroun wakiwa na Mke wake, Hii ilikua Dar Live Mbagala |
Karibu miaka 15 imepita tangu Inspektah Haroun kahena wa kundi la Gangwe
mob ai release ngoma yake ya Mtoto wa geti kali enzi hizo music videoz sio ishu
sanaaa mwaka 2000, sasa kwa wakati huu Inspeta akiwa ameshirikiana na Pro 24 wameshoot
video ya ngoma hiyo na inatarajiwa kutoka wakati wowote,
Kwa mujibu wa Inspekta Haroun anasema Video Queen katika Chupa
hiyo ni Wife wake mwenyewe, yani wife wake ndo mtoto wa Geti Kali, Video
imepigwa katika maeneo ya Temeke Mikoroshini sehemu ambako kundi la Gangwe Mob
lilizaliwa, pamoja na maeneo ya kishua ya Masaki.
Mtoto wa geti kali ili rekodiwa mwaka 1999 chini ya Producer Mika Mwamba wa fm Studios na ikatoka mwaka 2000, mpaka leo mwaka 2014 imepita miaka 15 tangu itoke na ni moja kati ya Ngoma ambazo zilivuma sana, kuweka alama kwenye historia ya muziki wa kizazi kipya.