WAIMBAJI
wa muziki wa Injili kwa mtindo wa kufoka
foka ‘Gospel Hip hop’ wameendelea kumuomba Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi
ya Tamasha la Pasaka, Alex Msama kutazama upande wao hasa mradi wa Yesu Okoa
Mitaa (YOM).
Kwa
mujibu wa mratibu wa mradi huo, George Rungu ‘Rungu la Yesu’ miondoko hiyo ya
kufoka foka nayo inashika kasi katika tasnia ya muziki wa Injili hivyo
waandaaji wa Tamasha la Pasaka waelekeze nguvu zao upande huo kwani wana idadi
kubwa ya mashabiki.
Rungu
la Yesu alisema kwa kuanzia wanampongeza Msama kwa kuandaa matamasha ya
kumtukuza Mungu kwani ni injili ya aina yake kwa sababu yanashirikisha imani
mbalimbali kwa lengo la kusaidia jamii zenye uhitaji maalum.
Rungu
la Yesu alisema wanampongeza kwa kile anachokifanya kwani anaowasaidia
wanamshukuru na Mungu anapokea dua zao.
Rungu
la Yesu alisema kwa sapoti anayotoa Msama katika nyanja mbalimbali za Kijamii
wako tayari kulisapoti tamasha la Pasaka kwa hali na mali kwa sababu
kinachofanyika kinagusa pande zote za jamii.
Tamasha la Pasaka linatarajia kuanza Aprili 20 jijini
Dar es Salaam ndani ya Uwanja wa Taifa.