Wednesday, October 12, 2016

Wazazi Wahusishwa Kifo Cha Mtoto Aliefunga Kwa Siku 68

Polisi India wanachunguza wazazi wa msichana mwenye umri wa miaka 13 aliyefariki wiki iliyopita baada ya kufunga kwa siku 68 kama ibada.
Police kusini mwa Hyderabad wameimbia BBC wanchunguza iwapo Aradhana Samdariya alilazimishwa kufunga.
Wazazi wake wanasisitiza kuwa alifunga kwa hiari kama inavyotakiwa katika Jainism, mojawapo ya dini.
Mkasa huo umesababisha mjadala kuhusui bada ya kufunga India.
Ripoti zinasema Aradhana alikunywa maji ya kuchemshwa tu kwa siku 68.
Siku mbili baada ya kusitisha kufunga wiki iliyopita, alifariki.
Wataalamu wanaamini binaadamu anaweza kukaa bila ya chakula kwa hadi miezi miwili.
Msemaji wa polisi amesema kesi imeanzishwa dhidi ya wazazi wa mtoto huyo baada ya shirika la kutetea haki za watoto kuwasilisha malalmiko.

Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.