Monday, March 31, 2014

YOU HEARD : WARAKA WA MTANZANIA ALIYEGEUZWA MTUMWA WA NGONO CHINA

Inasemekana eti huyu ndo Candy Baada ya Kufika China
Mwanadada mmoja wa Kitanzania anayetambulika kwa jina moja la Candy ambaye sasa hivi yuko nchini China akitumikishwa kwenye biashara ya Ngono yeye na wadada wenzake wa kitanzania wametuma waraka wa wazi wa sauti kwa Wizara ya mambo ya Nje na Watanzania kwa Ujumla akilalamikia kitendo cha baadhi ya kina mama wa kitanzania waishio China kwa vitendo vya kuwauza wakinadada wa Kitanzania ambao huwachukua bongo kwa kuwalaghai kuwa China kuna dili nyingi baada ya kuwachukua wakiwafikisha China wanawageuka kwa kuwanyang'anya Passport na kuwalazimisha wauze miili na malipo ya Biashara hiyo inaenda kwa wa mama hao, Waraka wa Candy na wenzake alioutuma nchini Tanzania kwa njia ya sauti unasome hivi

WARAKA

Ndugu Waziri Membe, Tunasikitika sana kwa haya yaliyotokea kwa sababu tumepoteza muda wetu mrefu sana kwa kuwafaidisha watu ambao wanatumia unyama kutufanyisha kazi ndugu zao ambao wengine ni dada zao wengine wadogo zao lakini wana force waitwe mama kwa ajili ya pesa zao na kutuuzisha miili kwa nguvu ili wapate wao pesa, na kutupokonya Haki zetu za msingi kama Passport ambayo hatakiwi kushika mtu ambae hausiki na Passport lakini wao wanatupokonya Passport zetu kinguvu na kuzishika wao, na mpaka sasa hivi tunasikitika hadi kuomba msaada ni kwamba tunahitaji mtusaidie kutukamatia hawa ambao wamepokonya Passport zetu na wamekimbia mpaka sasa hivi hatujui wapo wapi, kwa kuwa nyie ni mtandao wa serikali ni mkubwa tunahitaji kurudishiwa Passport zetu kwani tumepoteza muda tuna watoto wetu tumewaacha Tanzania tuna familia zetu tumekuja kutafuta maisha lakini tulichotegemea  sicho tulichokikuta ila tunaomba msaada tupate Passport zetu zirudi mikononi mwetu, kwasababu ajira zipo nyingi China hata kama tutaendelea kufanya kazi huku basi iwe rahisi kwa kuwa tutakua na Passport, China kuna kazi nyingi kama za kuuza Mama Ntilie za waghana au kuhudumia za wachinalakini wao wametulazimisha kufanya kazi yao ya Kujiuza, sisi hatupo tayari kufanya kazi hii ya Uharamu tutatafuta ajira nyingine kwa kutumia mikono yetu sisi tunapingana na umaskini na tunatambua ya kwamba vijana ndio nguvu ya taifa, tunaomba msaada mheshimiwa waziri Membe, hatukuja kwa lengo la biashara ya Ngono labda hao wa mama waliotutangulia hiyo ndio kazi yao kama huyo Mama anayeitwa Havintishi anayeuza mama ntilie katika mji wa Ghuang Zhou jengo moja linaitwa Tinshuu ghorofa ya Tisa wapo wengi sana ukienda katika ile ofisi utakuta wadada wengi sana. MWISHOOOOO

Mwanadada Candy kwa huku Tanzania yeye ni mkazi wa jijini Mbeya kwa Kina ndaga fijooooo, mwezi wa December mwaka jana 2013 alikutana na Dada mmoja huko Mbeya akamwambia kama yuko tayari amchukue waende China kwani kuna Mchongo wa Kazi za Umama Ntilie basi Candy pasi na kujua kuwa anaingia chaka akajikusanya na kuwaaga nduguze safari Ikaanza, kufika China Candy akafanyiwa bonge la shopping mwanadada akapendeza sanaaaaaaaaaaaaaaa
Ila baada ya Ile shopping ni maumivu mpaka leo kwani amenyang'anywa Passport na anauzwa mwili wake kwa kulala na wanaume na pesa ikiingia anaichukua tajiri yake.
Skiza Sauti ya Mwanadada huyo kama alivyotiririka kwenye You Heard ya XXL/Cloudsfm


Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.