Sultani na mtawala wa Brunei ambaye ni mmoja wa matajiri wakubwa duniani |
Serikali ya Brunei iliyo Kusini
Mashariki mwa Bara Asia, itaanza kutumia sheria kali za kiisilamu.
Kiongozi wa nchi hiyo ya kiisilamu
ambayo ni jirani na Malaysia ametangaza kuwa sheria hiyo itaanza kutumika
kuanzia wiki hii.
Adhabu zilizo chini ya sheria za
kiisilamu ni pamoja na kuwakata wezi mikono na kuwapiga mawe hadi kufa watu
waliopatikana na hatia ya kushiriki Zinaa.
Sheria hii itatekelzwa katika awamu
tatu katika kipindi cha miaka mitatu.
Umoja wa Mataifa tayari umeelezea
wasiwasi wake kuhusu sheria hiyo.
Taifa la Brunei tayari linafuata
sheria kali za kiisilamu kuliko hata nchi jirani kama Malaysia na Indonesia
pamoja na kuharamisha uuzaji na utumiaji wa pombe.
Nchi hiyo ndogo ilio katika kisiwa
cha Borneo,inatawaliwa na Sultan Hassanal Bolkiah na imepata utajiri wake
kutokana na kuuza nje mafuta na gesi yake.
Takriban nusu ya waisilamu wanaoishi
katika nchi hiyo ni raia wa Malaysia.
Sultani alinukuliwa akitangaza hatua
ya kwanza ya kuanza kutumiwa kwa sheria hiyo akimshukuru Mungu na
kuwatahadharisha wananchi kuhusu kuanza kutumika kwa sheria hiyo.
Sheria yenyewe itaanza kutumika
katika kipindi cha miaka mitatu huku hukumu ya makosa ya kwanza ikiwa kifungo
cha jela pamoja na kutozwa faini.
Katika awamu ya pili ndipo wahalifu
wataanza kukatwa mikono kwa watakaopatikana na hatia ya wizi , huku awamu ya
tatu ikihusu kupigwa mawe wazinifu na wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja.
Sultani anayetawala kisiwa hicho ni
mmoja wa matajiri wakubwa duniani na tayari amewaonya watu kukoma kushambulia
mipango yake kupitia mitandao ya kijamii.
Mfumo wa sheria katika mahakama
nchini humo ni sawa na ule wa Uingereza.
Umoja wa Mataifa uliitaka serikali
kuchelewesha mageuzi hayo ili kuhakikisha kuwa sheria hiyo inaambatana na
sheria za kimataifa kuhusu haki za binadamu.
Credits: BBC
Credits: BBC