|
Dudu Baya |
Kama jana ulisikiliza kipindi cha XXL au kupitia mtandao huu basi ulikutana na story ya Dudu Baya kumkata sikio mama yake mkubwa, kwa mujibu wa Mdogo wa kiume na DuduBaya alitiririka kuwa siku ya jumamosi iliyopita Jijini Mwanza Dudu alimvamia mama yake mkubwa na kumjeruhi kwa kumkata sikio kisha akatokomea kusikojulikana, sasa kwa jana Dudu alikua hapatikani kwa simu yake ya mkononi, ila leo Jibaba likapokea simu na kukanusha tuhuma hizo na kwa wakati huu yupo Shinyanga akifanya biashara zake, akaongeza kuwa hajaonana na mama yake mkubwa tangu mwaka 2001 na wala hajui anapoishi, Dudu alimalizia kwa kunihadithia story ndefu ya familia yao,
"Unajua nini? mimi nina wasiwasi na hawa ndugu zangu, Enzi nina hit na nyimbo kwenye vyombo vya habari mimi nikawa nina waintertain kwa kugawana nao pesa niliyokua naipata, lakini wakawa wananisema kwetu kuna hali ngumu na mimi sijajenga, basi nikaamua kujenga lakini kabla nyumba haijasha wakawa wanaleta maneno eti nyumba haitokamilika nitakua nimekufa kwa uchawi, sasa hao hao ndio ninao wahisi kuwa wanataka kunichafua kwa watanzania, na aliyeongea jana kweli ni mdogo wangu lakini tuhuma alizoongea kuhusu mimi ananisingizia, kama kweli natafutwa na polisi mbona sijapigiwa simu ili nikaripoti?