Friday, January 9, 2015

Jamaa hajafika kazini kwa miaka 24 na bado alikuwa mfanyakazi!

Huenda huku kwetu sheria zinabana zaidi kuhusu utaratibu wa kazi na ajira, sikuwahi kusikia story ya mtu kukaa miaka 25 bila kuhudhuria kazini na bado akawa na sifa ya kuwa mwajiriwa!
Mara nyingi kumekuwa na story watu wakisema kwamba eti ukipata kazi ya Serikalini ni ngumu sana kufukuzwa hata kama umefanya kosa kubwa kiasi gani, zaidi zaidi utahamishwa kituo cha kazi.
AK Verman, Mhandisi Mkuu katika Idara Kuu ya Kazi za Umma huko India, amefukuzwa kazi baada ya kutoonekana kazini tangu mwaka 1990.
Kesi yake ilianza mwaka 1992, alikutwa na hatia ya kutohudhuria kazini bila taarifa yoyote, lakini cha kushangaza ni kwamba imechukua miaka mingine 22 mpaka Baraza la Mawaziri lilipoingilia kati na kutoa maamuzi ya kumsimamisha kazi jamaa.
Serikali imebadilisha Sheria ya kazi, iliyopo sasa hivi imerahisisha zaidi kwa wafanyakazi kuajiriwa na kufukuzwa, Waziri Mkuu wa India, Narendra Modi amesaini Sheria hiyo kuanza kutumika pamoja na utaratibu mpya wa kusign kwenye mtandao kila unapoingia ofisini.

Comments System

facebook

Disqus Shortname

Powered by Blogger.