Saturday, May 3, 2014
BASATA WASHTUKIA UHALIFU KATIKA UPIGAJI WA KURA ZA KILI TANZANIA MUSIC AWARDS 2014
Wakati tukiwa tumebakiza masaa machache kufikia muda wa utoaji wa Tuzo za Tanzania, Mratibu Kili Tanzania Music Awards 2014 Kurwijira Ng'oko Maregesi amesema miongoni mwa changamoto ambazo wamezipata katika zoezi la upigwaji wa kura kwa wasanii waliokua nominated katika vipengele mbalimbali changamoto hiyo ni baada ya mitambo yao kumshtukia jamaa mmoja anayeishi Arusha kufungua Email 300, Kwirijira anasema email hizo zimefunguliwa kupitia server moja, hiyo inatokana na vigezo vya kupiga kuwa ni Email moja kwa kura moja kwa kila kipengele, hiyo ina maana kuwa mtu huyo alipanga kumpigia kura msanii mmoja kwa kura zote 300 kitendo ambacho ni kosa.
Comments System
facebook